Na Jane Edward, Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda ameitaka mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha Auwsa kutoa elimu kwa wananchi juu ya taarifa za miradi ya Auwsa ikiwa Ni pamoja na kuimarisha dawati la malalamiko ya wananchi.

Mtanda ameyasema hayo wakati akifungua kikao Cha wadau katika ushirikishwaji wa kukusanya maonii juu ya maandizi ya mkataba wa huduma kwa mteja kilichoandaliwa na mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha.

Amesema kuwa mamlaka inapaswa kutoa elimu kwa jamii kwani wananchi wanapaswa kuelewa taarifa zote za miradi ya maji kwa lugha nyepesi na namna bili za maji zinavyolipwa ikiwa Ni pamoja kuimarisha dawati la malalamiko.

Aidha mtanga ameisisitizia mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa wanakuwa na huduma nzuri ya mapokezi ya kuwasikiliza wateja vizuri ili kuwawezesha wananchi kuridhika na huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo Cha mawasiliano na huduma kwa wateja Auwsa Masoud Katiba akiwasilisha rasimu ya mkataba wa huduma kwa mteja katika kikao hicho amesema madhumuni ya mkataba huo Ni kuwawezesha wateja kujua huduma zinazotolewa na viwango vya huduma hiyo.

Aidha Katiba alisema kwa kutambua umuhimu wa mkataba huo wao kama mamlaka wameamua kuwaweka wananchi na viongozi wao wa kata ngazi zote  ili kusikiliza Changamoto na kuboresha huduma hizo

Ameongeza kuwa mkataba huo utafanywa na kitengo cha mipango na maendeleo na taarifa ya ufatiliaji wake ikiwemo ukiukwaji wa mkataba huo ambapo itawasilishwa Kila mwezi na kujadiliwa katika vikao vya menejimenti kwa ajili ya maamuzi.

"Mapitio ya mkataba huu yatafanyika kila baada ya miezi mitatu ambapo mkata huo utapitiwa kila kunapokuwa na mabadiliko ya sera, Sheria,kanuni na taratibu ambapo utaanza kutumika rasmi baada ya kupitishwa na bodi ya wakurugenzi ya mamlaka na kuidhinishwa na EWURA"alisema Katiba

Kaimu Mkurugenzi wa Auwsa Injinia Upendo Shushu alisema wananchi watarajie kuona mabadiliko ya utoaji wa huduma za mamlaka hiyo katika usikilizwaji wa wananchi mapokezi pamoja na mambo mengine lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna malalamiko ya ukosefu wa maji.

Katiba mkuu wa kitengo cha mawasiliano na huduma kwa wateja Auwsa akielezea kuhusu maandalizi ya mkataba wa huduma kwa mteja ili kuboresha huduma pamoja na upatikanaji wa maji safi Mkoa wa Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda akihutubia kikao cha  wadau wa maji Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...