Na.Khadija Seif,Michuzi Tv


WATANZANIA watakiwa Kupanda Miti kwa wingi Ili kuendelea kupata hewa ya oxygen Kwa wingi na kuendelea kutunza Mazingira.


Akizungumza na Michuzi mara baada ya Kupanda Miti katika Msitu uliopo pugu wa Kizimzumbwi ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Kutunza Mazingira (Green Initiative) Aidan Maga amesema mara Kwa mara wamekua wakishiriki kujitoa Kwa watu wenye uhitaji pamoja na kushiriki usafi wa Mazingira pamoja na kupanda Miti.


"Kampuni yetu imeanza vizuri Kwa mwaka huu na tumeshiriki zoezi la upandaji Miti katika hifadhi ya Kizimzumbwi takribani Miti 12 imepandwa lengo likiwa ni Kutunza Mazingira na kujiletea hewa ya oxygen Kwa wingi.


Hata hivyo Maga ameeleza sababu ya kushiriki upandaji wa Miti ni kutokana na Hifadhi hiyo kuwa sehemu ya Dar es salaam yenye Makazi ya watu wengi hivyo kulazimika wakazi hao kuhitaji hewa ya kutosha.


"Hifadhi hiyo inahitaji kutoa hewa ambayo wakazi wa Dar es salaam wanalazimika kuhitaji hivyo zoezi la upandaji Miti utachangia Kwa kiasi kikubwa kuzalisha hewa ya oxygen Kwa wingi na kupitia (Green initiative ) tunaendeleza Kampeni ya upandaji Miti Kwa wingi."


Pia ameeleza kuwa Matarajio ya Kampuni hiyo kutembelea Mkoa wa Tanga Kupanda Miti Kwa wingi kwani Kuna baadhi ya sehemu hazijapewa kipaumbele kwenye swala la Kutunza


Baadhi ya wadau wa Mazingira kutoka Kampuni ya Green Initiative wakishiriki zoezi la usafi katika Msitu uliopo pugu wa Kizimzumbwi lengo likiwa ni Kutunza Mazingira katika Msitu huo katika Jiji la  Dar es salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Green Initiative akiwa pamoja na wafanyakazi wa Kampuni hiyo mara baada ya kutembelea Msitu uliopo pugu wa Kizimzumbwi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...