Na Khadija Kalili , Chalinze
NAIBU Waziri wa Wizara ya Ardhi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ametoa shukran za dhati kwa niaba ya wananchi wa Jimbo hilo baada ya kupatiwa mikopo ya miradi ya kmikakati ambayo itawawezesha wananchi hao kutoka katika makundi ya Wanawake, Walemavu na Vijana yenye lengo la kuwawezesha katika nyanja za kuwainua kiuchumi.

Mheshimiwa Kikwete amesema hayo Jana katika makabidhiano ya pikipiki 12 zilizotolewa na Halmashauri ya Chalinze kwa mkundi yafuatayo ambayo ni Maafisa Ugani ambao wamepewa vitendea kazi hivyo Ili waweze kurahisisha shughuli zao za kila siku.

Aidha kundi la Walemavu na Vijana walupatiwa mikopo ya pikipiki huku kundi la wanawake wakipatiwa mkopo wa gari aina Noah vyote vikiwa na thamani ya

"Kwa niaba ya Wanachalinze natoa shukran zangu za dhati kwa Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu kwani haya yote yanatokea kwa kutimiza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inyoelekeza kuwajali na kuwatumikia wananchi ipasavyo"alisema Mheshimiwa Kikwete.

"Hivyo basi kwa niaba ya Wanachalinze niseme Rais wetu Mama Samia anatekeleza kwa vitendo ahadi zake kwao pia napenda kumshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Hassan Mwinyikondo , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze na Wataalamu wote kwa ujumla kutokana na jinsi wanavyoipeleka Chalinze katika maendeleo kwa mwendo wa kasi na tunaoutaka Wanachalinze" alisema Mbunge huyo wa jimbo la Chalinze.

Aidha ametoa rai kwa wananchi n makundi ambayo hawakufanikkwa kupata mikopo hiyo kwani huu ni mwanzo hivyo wavute subira wakati wao utafika huku akiwasisitiza makundi hayo waliofaidika na mikopo hiyo kyihesgimu na kuirejesha kwa wakati Ili makundi mengine yaweze kukopeshwa.
Wakati huohuo Halmashauri ya Chalinze imetoa pikipiki kwa Maafisa Ugani ambazo imeelezwa kuwa zikawaweshe katika.utendaji wao wa kazi za kila sku na siyo vinginevyo.

Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah aliwaambia Maafisa Ugani kuwa wakazitunze pikipiki hizo kwani siyo chanzo Cha kuniongezea kipato au kuzifanyia biashara (Bodaboda) kwani wamepewa Ili waweze kuitumia jamii ipasavyo.

DC Zainab alisema kuwa pikipiki hizo zimenunuliwa kutokana na mapato ya Halmashauri ya Chalinze yatikanayo n makusanyo ya fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali .

Aidha DC Zainab aliongeza kwa kusema kuwa utaanzishwa mpango wa kuweka makambi kwa wanafunzi huku lengo ni kupandisha ufaulu kwa wanafunzi wake sanjari na kuwataka wazazi wote kuchangia mpango wa chakula mashuleni kwa sababu imebainika njaa ndiyo chanzo kutofanya vizuri wanafunzi.

"Nataka kila mzazi achangie fedha kwa ajili ya chakula cha mtoto na kwa mzazi atakayekaidi kumtolea mtoto pesa ya mchango wa chakula nitakula nao sahani moja tuwekeze nguvu katika.masomo kwa kuwapatia wanafunzi chakula"alisema DC Zainab.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...