MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amewavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123 waliotunukiwa nishani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Akisoma taarifa ya kuvisha nishani hizo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela, amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa mamlaka aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ametunuku nishani ya miaka 60 ya uhuru, nishani ya utumishi uliotukuka na nishani ya utumishi mrefu na tabia njema.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, akiwavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123 jijini Dodoma Januari 22, 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...