Na.Khadija Seif, Michuzi TV


KLABU ya Jeshi ya Gofu Lugalo Kwa kushirikiana na Kampuni ya Serengeti brewis kupitia kinywaji cha John walker wadhamini Shindano la "Johhnie Walker Waitara Trophy" linalotarajiwa kufanyika januari 29 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi Wahabari wakati wa kutambulisha Mashindano hayo Mwenyekiti wa Klabu Bregedia Michael Luongo amesema Mashindano yana lengo la kumuenzi Muasisi wa Klabu ya lugalo gofu Mstaafu Jenerali George Waitara.

"Shindano hilo lilitakiwa kufanyika mwaka Jana lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo Mashindano hayo yatafanyika mwaka huu Kwa ajili ya heshima Kwa Muasisi wa Klabu ya Lugalo Waitara".

Aidha ameeleza kuwa Mashindano hayo yatashirikisha wachezaji kutoka Klabu zote za hapa nchini kama vile Moshi club,Arusha Gymkhana, Mufindi Club, Morogoro Gymkhana,Dar es salaam Gymkhana,Sea Cliff Golf Club kutoka Zanzibar,Kili Golf na Tpc golf club.

Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Jeshi ya Gofu Lugalo Meja japhet Masai amesema Mashindano hayo yatakua ni siku Moja ambapo wachezaji watacheza Mashimo 18 Mfumo wa Neti na Wachezaji kutoka Vilabu vingine wanakaribishwa kushiriki Mahsindano hayo.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Serengeti breweries Lumuli Minga amesema Kampuni hiyo imetoa udhamini Kwa mara ya 3 mfululizo na hawatasita kuendelea kutoa udhamini kwenye Mchezo wa Gofu.

"Michezo Ina nafasi kubwa katika Taifa letu hivyo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo imelazimika Mashindano haya yafanyike Kwa mwaka huu na hututosita kuendelea kutoa udhamini wetu kwenye Miche hii na mengine."

     Nahodha wa klabu ya Lugalo Golf, Meja Japhet Masai akizungumzia maandalizi kuelekea mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy ambapo wataanza na shindano la  wachezaji wa kulipwa ambao watacheza siku ya Ijumaa na wachezaji  wa ridhaa kwa maana ya Div A,B,C, Seniors,na Ladies watacheza siku ya Jumamosi Januari 29. 
 Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Lumuli Minga akikabidhi moja ya kikombe kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo,Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuelekea kuanza kwa mashindano ya Johnnie Walker Waitara Trophy yanayotarajiwa  kutimua vumbi  Januari 29 mwaka huu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...