Na Mwandishi wetu, NCAA.

Katika jitihada za kuendela kutangaza vivutio vya utalii kwa Watanzania timu ya NCAA imetembelea vyuo vikuu vilivyopo Zanzibar na Iringa kwa lengo la kutoa hamasa kwa wanafunzi wa vyuo vya kati na Vyuo vikuu kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko eneo la Hifadhi ya Ngorongoro hasa wakati wa likizo.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Afisa Uhusiano wa Masoko Mtandao wa NCAA Bw. Samwel Nsyuka pamoja na kuhamasiaha utalii wa ndani pia imelenga kutoa elimu na kupima uelewa kwa vijana wa vyuo vikuu kuhusu Uhifadhi, Utalii wa utamaduni, malikale, miamba na na maliasili zinazopatikana katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

“Ziara yetu ya kutembelea vyuo vya kati na Vyuo vikuu ni utekelezaji wa mpango mkakati wa NCAA kutoa hamasa kwa wanafunzi na watu wengine kutembelea vivutio vyetu kila wanapopata fursa lakini pia kutoa uelewa wa masuala ya Uhifadhi, utalii wa mambo kale na utalii wa Miamba” aliongeza Bw. Nsyuka.

Ameongeza kuwa mbali na kutembelea wanafunzi vyuoni pia timu hiyo kwa upande wa Zanzibar imekutana na wageni mbalimbali walioko katika maeneo ya fukwe za Nungwi na Mji Mkongwe na kuwaeleza fursa  za vivutio vya utalii vinavyopatikana Tazania bara.

Katika kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa upande wa Zanzibar timu ya NCAA pia imekutana na wanafunzi wa vyuo vikuu vya The State University of Zanzibar (SUZA), Zanzibar University (ZU) pamoja na Chuo cha Utalii Maruhubi.

Wakufunzi na Wanafunzi mbalimbali wanaosoma katika vyuo hivyo pamoja na kuhamasiska na utalii wa ndani wengi wao wameoonyesha kuwa na uelewa kuhusu vivutio vya utalii vilivyoko Ngorongoro na kuomba kupatiwa uelewa wa namna bora ya wao kuvitembelea kutokea Zanzibar ambapo timu ya NCAA imetumia fursa hiyo kutoa utaratibu na kuwaunganisha na wadau wa usafiri wa watalii kutoka Zanzibar kwenda Ngorongoro.

Katika kupanua fursa za Utalii kwa Zanzibar kutembelea Ngorongoro timu ya NCAA pia imekutana na wadau wanaohamasisha safari za wageni walioko Mji Mkongwe na Nungwi ili kuwaomba kuwa mabalozi wa kuhamasisha utalii wa vivutio vilivyoko NCAA na kuleta wageni Tazania Bara hususan Ngorongoro.

Kwa upande wa Tanzania bara timu ya umamashishaji wa Utalii kutoka NCAA imemetembelea Chuo Kikuu cha Ruaha pamoja na chou kikuu cha Iringa kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa Ndani na kutoa ellimu kuhusu Uhifadhi, utalii wa wanyamapori, miamba, Utamaduni na malikale.

Bw. Samwel Nsyuka kutoka NCAA (wa tatu kutoka kushoto) akiwa Pamoja na wanafunzi na Wakifunzi katika chuo Cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakifurahia bidhaa mbalimbali (Promotion Maretials) za Kutangaza Utalii wa NCAA




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...