Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC)  Bw. Mathew M. Kirama amewapongeza Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR MUUUB), Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb), Naibu Waziri (OR MUUUB), Dkt. Laurean J.P. Ndumbaro, Katibu Mkuu (OR MUUUB) na Bw. Xavier M. Daudi, Naibu Katibu Mkuu, (OR MUUUB) kwa kuaminiwa kwao na kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Tume, Bw. Mathew M. Kirama amesema kupitia salamu za pongezi alizozituma kwao kuwa Menejimenti na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma  wanawaahidi ushirikiano na kuchapa kazi, kazi iendelee.

Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. (Pamoja na marekebisho ya mwaka 2019).

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...