Mhadhiri Msaidizi idara ya Ustawi wa Jamii Taaluma ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii Bi.Rufina Khumbe akifungua kongamano la kumjengea binti uwezo kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni lililofanyika katika ukumbi wa maktaba wa Taasisi hiyo mwishoni mwa juma hili Jijini Dar es Salaam.



OWESOME YOUTH VISION GROUP chama cha wanafunzi wa Kike wa  Taasisi ya Ustawi wa Jamii kijitonyama, Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum  leo wamefanya Kongamano la mabinti maalumu kwa kumjengea mtoto wa kike. 

Kongamano hilo lilifunguliwa na Mhadhiri Msaidizi Kutoka idara ya Ustawi wa Jamii taaluma Rufina khumbe kwa niaba ya mkuu wa Taasisi Dkt.Joyce. Nyoni. 

Akiongea wakati wa kufungua kongamano hilo Bi Rufina alisema thamani ya mwanamke ni asili kupitia maandiko ambapo Mungu alibaini uhitaji wa Mwanamke na ndipo akamtengeneza mwanamke kukamilisha uumbaji, kibali na baraka za Mwanaume na jamii  zipo kwa mwanamke hivyo binti ni dhahabu, binti ni lulu.

Thamani yake ni kubwa sana katika dunia hii, anapaswa kujitambua, kujithamini na kuachilia zile baraka ambazo mungu amempatia kwa kufanya yaliyo mema na kukubalika na jamii yake. 

Lengo kuu la kongamano hilo ni Kumnyanyua binti; kwa kumpa elimu na kumjengea uwezo wa kujitambua na kuwa na ujasiri wa kuthubutu na  kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na Elimu , uongozi, kupaza sauti kwa niaba ya mabinti wenzie, kujiamini na kujisimamia  pamoja na ujasirimali.

Sambamba na hilo pia wanafunzi wa kike wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii walipatiwa elimu kuhusiana na nidhamu, elimu na maisha ya chuo kwa kipindi ambacho wapo Taasisi na namna sahihi ya kuweka malengo, nidhamu na namna ya kukabiliana na changamoto za mazingira, na kuweza kufikia malengo alisema Mhadhiri Rufina.

Mada mbali mbali ziliwasilishwa na wachangia mada waalikwa ambapo "Elimu juu ya haki na usawa wa kijinsia"  iliwasilishwa na mwalimu  Sophia  Mbeyela kutoka Shule ya Msingi Kijitonyama. 

Vile vile mada kutoka kwa  mkurugenzi  wa Amani Project ambayo inahusisha watu wenye uhitaji maalum. 

Elimu ya Afya  na maadili ambayo iliwasilishwa vyema na  ndugu Asumpta Godfrey ambaye ni mwanzilishi wa Be Hamble project na mtangazaji wa redio.

Sambamba na hayo elimu juu ya binti kutambua fursa na kuzitumia  hasa anapokuwa chuo na namna sahihi ya kujiwekea malengo na kuhakikisha kufikia malengo ambapo ilitolewa  vyema na ndugu Asma Jamida kutoka wasafi media.

Kwa upande wake  Shamira Mshangama kutoka Wasafi Tv alizungumzia uongozi na mwanamke namna ambavyo binti anaejitambua, kujithamini na kujiwekea malengo anaweza na kuwa kiongozi bora kutoka ngazi ya Taasisi hadi Taifa 

Nini afanye na nini kuepuka,  mbinu na taratibu za kufanya; changamoto na namna yakukabiliana nazo. 

Taasisi ya Ustawi wa Jamii inatambua nafasi kubwa iliyonayo ya kutoa elimu bora ya kitaaluma kwa wanafunzi inayowaandaa kuhudumia jamii  lakin pia Kutoa elimu kwa Jamii inayozunguka Taasisi  na Jamii ya watanzania kwa ujumla ili kupunguza matatizo ya Kijamii ya mtu mmoja mmoja, familia, na Makundi maalum kama ambavyo Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano  wa Tanzainia  Samia Suluhu aliona upekee katika ustawi wa jamii na kuunda  Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambayo Taasisi ya Ustawi wa Jamii iko chini yake.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii itaendelea kumuunga mkono Mh. Rais Samia kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia Vyombo vya habari, vyumba vya mihadhara ya kitaaluma na Kituo chake cha Elimu, Ushauri na Msaada wa kisaikolojia  pamoja na mikutano na wanajamii ili kupunguza vitendo viovu na vya ukatili kwa Watoto, wanawake na makundi maalum vinavyoendelea  kushamiri hapa nchini.

Mwalimu wa shule ya Msingi Kijitonyama Mwl.Sophia Mbeyela akitoa wasilisho katika kongamano la kumjengea binti wa kike uwezo lililofanyika mwishoni mwa juma katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam.
Watoa Mada na baadhi ya wanafunzi walioshiriki kongamano la kumjengea binti uwezo katika picha ya pamoja mwishoni mwa juma mara baada ya kufanyika  kongamano hilo  katika ukumbi wa maktaba wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama Jijini Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...