Adeladius Makwega-Moshi
MACHIFU U wa Mkoa KilimanjAro kwa pamoja wamesema kuwa maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la Kilimanjaro yamekamilika vizuri na wapo tayari kumpokea Mgeni Rasm Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

Jeremia Senduia Laizer ambaye ni Olegwanani wa Wamasai wa Kilimanjaro amesema kuwa japokuwa jambo hili ni geni lakini muitikio umekuwa mkubwa sana.

“Hivi sasa sisi tupo tayari kumpokea Mkuu wetu wa Machifu Chifu Hangaya ambaye ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.”

Naye Chifu wa Wapare Gabriel Msofe amesema kuwa hata kwao wananchi wamehamasika mno kwani wametayarisha vikundi kadhaa vitakavyotumbuiza katika tukio hilo.

“Tumelichukua kwa uzito wa mkubwa Tamasha la Utamaduni la Kilimanjaro na ndugu zetu wa Upareni wanatamani kushiriki katika tamasha hili lakini ni mbali na gharama ndiyo maana sisi na wenzetu kadhaa tutawakilisha vizuri.”

Wakiwa kandoni mwa kikao maalumu cha maandalizi chini ya Uenyekiti wa Chifu Mkuu wa Wachaga Frank Mareale, kwanza alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri huku akikumbusha historia ya uchifu nchini Tanzania.

“Hapo awali serikali ilipofuta uchifu, tulidhani ilifuta hadi utamaduni na jambo hili lilififisha mno mambo ya kimila laikini kumbe ilifuta mambo ya Uhakimu na Utawala tu lakini Utamaduni ulibaki na ndiyo maana tulirudisha Umoja wa Machifu nchini na ndiyo maana sasa tunaweza kufanya tamasha kama hili la utamaduni.”

Chifu Mareale amesema kuwa mambo kadhaa ya kimila yatakuwepo katika tamasha hilo ikiwamo Ngesi, Mbege na Dengelua.

Tamasha Utamaduni la Kilimanjaro litafanyika Jumamosi ya januari 22, 2022 katika Viwanja vya Chuo Cha ushirika Moshi tangu saa moja ya asubuhi chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti wa Chifu Mkuu wa Wachaga Frank Mareale katikati akizungumza wakati w kutambulisha tamasha la Utamaduni la Kilimanjaro litakaloanyika Jumamosi januari 22, 2022.
Laizer, Mereale na Msofe wakiwa kwenye kikao cha machifu.
Wajumbe wa machifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...