Na John Walter-Manyara


Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), umefadhili Minara ya makampuni ya mitandao ya simu 54 katika kata 42 Mkoani Manyara.


Hayo yamesemwa na Mhandisi Mwandamizi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote, Baraka Elieza, wakatika akizungumza na Waandishi wa habari Mkoani hapa katika  ziara ya Naibu waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari amesema kuwa Minara yote walioifadhili imekamilika isipokuwa Minara miwili ambayo itakamilika mapema mwaka huu.


Ameitaja Minara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni ni katika Kijiji cha Sigino  pamoja na Kijiji cha Himiti.


Akizungumzia mipango ya mfuko huo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), kwa mwaka wa fedha 2021_2022, nikutekeleza ujenzi wa Minara katika kata 15 ndani ya mkoa wa Manyara.


Amesema wamejikita katika maeneo ya vijijini na baadhi ya maeneo ya mijini, ambapo Kuna usikivu hafifu wa mawasiliano, kwa kutoa ruzuku kwenye makampuni ya mitandao ya simu ili wapeleke huduma ya mawasiliano kwa wananchi, pamoja nakupeleka mawasiliano ya redioni katika maeneo ambao Kuna usikivu hafifu wa redio.


Aidha mfuko huo unafundisha walimu Mafunzo ya tehama, ili waweze kupata ujuzi, pamoja nakupeleka kompyuta katika shule za serikali, ikiwa lengo nikuunganishe shule hizo na intaneti.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...