*Asimulia changamoto ya Miaka mitatu kumpata Mpishi wa Kimataifa chief Tuba*
Na.Khadija Seif, Michuzi TV


WATAYARISHAJI wa Keki na vitafunwa wametembelea kiwanda cha Azam buguruni wakiwa na Mpishi wa Kimataifa chief Tuba kutoka Uturuki.

Akizungumza na Michuzi, Muandaaji wa Matamasha ya Keki Zena Sharif Scaba amesema Kampuni hiyo ya Azam ni Mmoja ya Mdhamini Mkuu wa Darasa la uokaji ambalo litachukua siku 4 likiwashirikisha Waokaji mbalimbali  wa ndani na ya nchi.

"Tumetembelea kiwanda cha Azam ambao wanazalisha unga Kwa ajili ya Mapishi mbalimbali hivyo imewapa fursa Waokaji kuona Maandalizi ya awali jinsi unga unavotengenezwa hatua ya mwanzo Hadi mwisho."

Hata hivyo Zena amefafanua zaidi jinsi alivyotumia miaka mitatu kumpata Mpishi huyo wa Kimataifa kutoka Uturuki na kumkubalia kuendesha darasa hapa Tanzania.

"Nilimuona kwenye Mitandao nikavutiwa na ujuzi wake wa jinsi anavyotengeneza keki za vitu mbalimbali na takribani miaka mitatu nimekua nikizungumza nae hivyo nikaona ipo haja ya yeye Kuja Tanzania kuwafunza wapishi Ili tunapoelekea Maandalizi ya Shindano la keki la Afrika Mashariki basi tuwe na kitu tofauti pamoja na kuleta Mabadiliko kwenye Soko la Keki na mvuto Kwa walaji Keki."

Pia Zena ameongeza kuwa sababu inayopelekea Waokaji kutoweza kutengeneza keki za maumbo ni kukosekana Kwa baadhi ya vifaa pamoja na rangi zinazoleta uhalisia zaidi na zaidi baada ya Mafunzo angetamani kutengeneza keki yenye sura ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu kama sehemu ya kuthamini kile anachokifanya katika nchi yetu.

Kwa upande wake Mmoja ya washiriki wa Darasa la uokaji Tamara Hashim kutoka Mkoa wa Arusha amempongeza Zena Kwa kuwapa fursa Waokaji kuongeza ujuzi kwenye upishi wa keki na kuwakutanisha na Mpishi wa Kimataifa.

"Ni fursa yenye lengo la kutuinua Waokaji na kupitia darasa hili tunategemea mengi zaidi na oda nyingi kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani ya nchi."
Picha ya pamoja kati ya Muandaaji wa Shindano la Keki Zena Sharif Scaba, Mpishi wa Kimataifa wa Keki zenye Maumbo mbalimbali Chief Tuba akiwa na Msaidizi wake pamoja na Mshindi wa Shindano la Cake off competition 2018 Alexander vitalis mara baada ya kutembelea kiwanda cha Azam buguruni

Mmoja ya Waokaji wa Keki kutoka Arusha Tamara Hashim akifafanua zaidi mategemeo yake baada ya Darasa hilo la Kutengeneza keki Kwa maumbo yatakavyomnufaisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...