Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amezitaka Taasisi za fedha nchini kutoa mikopo kwa wakati na kwa kuendana na misimu ya kilimo ili mkopo unaotolewa uweze kukidhi  dhumuni husika.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 28 Januari, 2022 alipokuwa Kilombero Mkoani Morogoro kushiriki kikao cha viongozi wa vyama vya ushirika wa miwa na Taasisi za fedha.

"Mabenki jitahidini kuendana na msimu au kalenda ya kilimo ili mikopo yenu iweze kutoka kwa wakati na kuwa na tija kwa wakulima wetu. Ninawashauri na kuwaomba muende mkajitafakari na kuja na mfumo wa utoaji mikopo utakaorahisisha huduma, kupunguza muda wa uchakataji na kuongeza tija kwa wakulima.

Lengo la kikao hichi ni kujadiliana kwa uwazi njia rahisi za kumkopesha mkulima wa Tanzania pasipo kuathiri masharti ya  kibenki, mfumo wa makubaliano ya utatu (Tripartite Agreement) kati ya Mkulima, Mwenye kiwanda (Mnunuzi) na Benki (Mkopeshaji) umerahisisha sana upatikanaji wa mikopo kwa wakulima tofauti na ule wenye hitaji la dhamana ya mkopo” Alisema Mavunde

Akitoa salamu za wananchi wa Majimbo ya Mikumi na Kilombero, kwa niaba ya Mbunge Abubakar Asenga wa Kilombero, Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mh. Dennis Londo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa utatuzi wa changamoto za wakulima wa Bonde la Kilombero ikiwemo kuanza kwa taratibu za awali za ujenzi wa daraja la Bonde la Mto Ruhembe ambalo lilikuwa kikwazo katika usafirishaji wa malighafi ya miwa kwenda katika kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

Wakati huo huo viongozi wa vyama vya ushirika wamepongeza kitendo cha Serikali kuja na mfumo wa kupanga maeneo ya uvunaji kwa zone (Zoning) ambao umeondoa kero kubwa iliyokuwa inawakumba wakulima wa Kilombero. Hali hiyo ilipelekea Mhe. Mavunde kuielekeza Bodi ya Sukari Tanzania kwa kushirikiana na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa kuhakikisha maeneo yote yenye wakulima wadogo wa miwa yanapangwa kwa kutumia mfumo huo.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...