Muonekano wa nyumba za makazi Magomeni Kota. Jijini Dar es Salaam.

* Wakazi watakiwa kutunza miundombinu ya nyumba hizo

UJENZI wa nyumba za makazi Magomeni Kota umekamilika kwa asilimia mia moja huku ikitegemewa kuhamiwa na wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika makazi hayo kabla ya Serikali kufanya ujenzi wa makazi hayo ya kisasa yakihusisha huduma muhimu ikiwemo maduka na Soko.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua nyumba hizo Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia Ujenzi Balozi, Mhandisi. Aisha Amour amesema baada ya kutembelea nyumba hizo kwa ufuatiliaji amejiridhisha kazi imekamilika na maboresho madogomadogo yanafanyika na muda wowote kuanzia sasa wakazi halali watahamia katika nyumba hizo na kuishi kama Serikali ilivyoahidi.

Amesema uwekezaji huo uliofanywa na Serikali ni mkubwa hivyo wakazi wa nyumba hizo lazima walinde miundombinu  ya nyumba hizo ili kuipunguzia gharama Serikali kwa kufanya marekebisho.

''Tumeona hapa miundombinu yote ipo salama na imara, wakazi watakaoishi hapa ni vyema wakaitunza miundombinu hii ili Serikali itumie fedha kuendelea kuboresha makazi ya wananchi kote nchini na miundombinu iliyowekwa itumiwe kwa matumizi yaliyobainishwa ikiwemo soko na sehemu ya maduka.'' Amesema.

Awali akieleza juu ya mradi huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania Arch. Daud Kondoro amesema makazi hayo  na uhakiki wa wakazi 644 wanaotarajiwa kuishi hapo umekamilika.

''Ufungaji wa lift kumi zitakazotumika katika majengo haya umekamilika, kuna sehemu ya uwekezaji wa maduka sakafu mbili unaendelea, kuna vizimba 186 katika uwekezaji wa soko pamoja na vyoo vya kulipia.'' Amesema.

Arch. Kondoro amesema, utekelezaji wa mradi huo umezingatia viwango vya hali ya juu na rasilimali za tofali na zege iliyotumika katika ujenzi huo ni zao la kiwanda kilichopo katika makazi hayo chini ya Wakala hiyo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia Ujenzi Balozi, Mhandisi. Aisha Amour akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi huo na kueleza kuwa amejiridhisha kazi imekamilika na maboresho madogomadogo yanafanyika, leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania Arch. Daud Kondoro akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo na kueleza kuwa  makazi hayo  na uhakiki wa wakazi 644 wanaotarajiwa kuishi hapo vimekamilika na wakazi hao watahamia muda wowote kuanzia sasa, leo jijini Dar s Salaam.



Ziara ikiendelea.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...