Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw'ilabuzu Ludigija akizungumza wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria Kanda ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yakitanguliwa na maandamano kuanzia viwanja vya Mahakama Kuu hadi Kisutu.
Jaji Mfawidhi mahakama kuu kanda Dar es Salaam,  Amir Mruma akizungumza wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria Kanda ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yakitanguliwa na maandamano kuanzia viwanja vya Mahakama Kuu hadi Kisutu.

SERIKALI imeitaka mahakama kwa kushirikiana na vyombo vyote husika kuondoa mashauri yote yaliyopo mahakamani ambayo hayana ushahidi ama ushahidi wake umechukua muda mrefu ili kupunguza mlundikano wa watu magerezani na pia kupunguza kazi zisizokuwa na mantiki kwa majaji.

Hayo yamesemwa leo Januari 23, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw'ilabuzu Ludigija wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria Kanda ya Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yakitanguliwa na maandamano kuanzia viwanja vya Mahakama Kuu hadi Kisutu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Dalaam, Ludigija amesema magereza yana mahabusu wengi ambao wanaipa serikali mzigo mkubwa.

" Tunatambua watu wamekaa magerezani lakini kwenye magereza yetu mtu akiwa mahabusu hafanyi kazi yoyote hivyo tunaongeza mzigo mkubwa kwa serikali usiokuwa na msingi amesema.

"Niwaombe sana  muondoe kesi zote zisizokuwa na ushahidi ili kupunguza mlundikano wa watu gerezani na pia kupunguza kazi zisizokuwa na mantiki kwa majaji na hatimae waweze kusikiliza kesi zenye ushahidi kwani magereza yetu wamejaa watu ambao wengine hawana sifa za kuwa gerezani, amesema Ludigija.

Aidha, Ludigija ameipongeza mahakama kwa kuendesha mashauri mengi na mengine yakiwa yanaendelea kwa njia ya mtandao kwani imesaidia kupunguza mlundikano wa mashauri yaliyopo na kubarikiwa na asilimia 15 tu za mashauri ambayo yamekaa kwa muda mrefu na mahakama imezidi kuayamaliza kwa mwaka huu.

Amesema, katika kipindi cha nyuma walikuwa wanapokea malalamiko kwa wananchi juu ya kesi zao ama kuchelewa ama uamuzi kutokuwa wa haki  lakini kwa sasa hakuna malalamiko hayo isipokuww yamebakia malalamiko kwenye mabaraza ya Ardhi.

Amesema, kuna changamoto kubwa kwenye kesi zinzohusiana na ardhi hivyo anawaomba Wanasheria na mawakili waangalie Uwezekano wa kuboresha.

"Kumekuwa na changamoto sana kwenye kesi za ardhi hasa kwenye mabara, mahakama iangalie hilo na kama kuna uwezekano  uwezokano basi waweze watu wengine ambao wako kisheria zaidi, ila pia naomba kama kuna namna ya kuweka kwenye mlolongo  mahakama za kawaida hizi kesi za Ardhi zingesaidia Sana. Kuwe na mabadiriko ikiwezekana kuwa na wanasheria waliosomea kabisa ili waweze kusaidia eneo hilo ambalo limekuwa na changamoto kubwa" amesema Ludigija.

 Amesema, Licha ya maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali pamoja na mahakama ya kuboresha miundombinu za majengo ya mahakama, bado kuna changamoto mbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya mahakama kama vile Mahakama ya Temeke na ya Jiji kutumia  majengo ya serikali. Tutakaa wakurugenzi kuona namna tunanaboresha mahakama hizo. 

 Aidha, awetoa wito kwa wapelelezi wote wa mkoa kuhakikisha wanafabya upelelezi mapema kabla ya shauri halijapelekwa mahakani isipokuwq kwa mashauri ya  matukio  ambayo sio ya kusubiri kwanza upelelezi ukamilike ndipo mtu afikishwe mahakamani kama vile mashauri ya mauaji kulawiti na mengineyo ambayo upelelezi wake huchukua muda mrefu, na iwapo mtuhumiwa atakaa nje anaweza kudhurika.

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi mahakama kuu kanda Dar es Salaam,  Amir Mruma amesema, katika wiki hii ya sheria ambayo inaashira kuanza mwaka mpya wa mahakama, watatoa elimu kwa umma kuhusu sheria haki zake katika kiwango cha msingi ili mwananchi atakayependa sue haki zake.

Jaji Mruma amesema, pamoja na mambo mengine wananchi wanapaswa waelewe kuwa dhana ya haki ni kushinda panapostahili na kushindwa unapostahili, Mwananchi anaposhinda kesi aridhike kwa kuwa haki ndivyo ilivyo na hata pale anaposhindwa kesi na akahukumiwa basi aridhike ndani ya Moyo wake kwa sababu hiyo pia ni haki na ndivyo palivyo.

Vile vile amesema, hata kwa upande wa Teknolojia kuna hasi na chanya zake, hivyo amewashauri wadau wote wakati wa kuchakata ushahidi waangalie sana Teknolojia maana inaweza kupotosha ukweli.

"mfano kwenye mitandao ya Kijamii kuwa kuna  uwezekano wa kumuona mtu unayemfahamu lakini kwa uhalisia siyo yeye, tuwe makini kuitumia Teknolojia kwa uchanya wake na Kuipuuza pale ambapo imetumika Kwa hasi yake.

Aidha ameongeza kuwa, utoaji huduma kwa njia ya Tehama umesaidia katika upatikanaji haki , kuongeza uwezo kupunguza gharama mbali mbali na kuondoa vitendo vya rushwa.

"Katika Kanda ya Dar es Salaam zaidi ya mashauri 1871 kati ya 2225 yalisajiliwa kwa njia ya mtandao ambayo ni sawa na 84% huku kwa mwezi Desemba pekee mashauri 798 yalisikilizwa kwa video conference na kuifanya Kanda ya Dar es Salaam kuongoza kwa kusikiliza esikiliza mashauri mengi kwa mwezi huo wa Desemba na kufikia 6352.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...