Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali inaunga mkono jitihada zote za kutangaza na kukuza lugha ya Kiswahili ili kuhakikisha inafahamika na kuzungumzwa duniani kote.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika, tukio iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mhe. Kassim ameagiza kuwepo siku ya Kiswahili Kitaifa ili kuithamini lugha hiyo wakati wa kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani, Julai 7 kila mwaka.

Pia, Waziri Mkuu ameipongeza Kampuni ya ALAF, Tanzania na Mabati Rolling Mills waliodhamini shindano la Fasihi ya Kiswahili kwa kengo kubwa la kuitangaza na kuendeleza lugha adhimu ya Kiswahili duniani kote.

“Ninatoa wito kwa Makampuni hapa nchini kuiga mfano huu kwa kuwekeza katika lugha ya Kiswahili huku tukitambua kuwa uwekezaji wa namna hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya biashara zetu na taifa letu kwa ujumla”, amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohammed Mchengerwa amesema Kampuni ya ALAF Tanzania imefanya jambo jema na linastahili kuungwa mkono na kila mdau wa maendeleo nchini ili kufanikisha azma ya Serikali kuitangaza na kukuza lugha ya Kiswahili sehemu mbalimbali duniani.

“Kwa sasa lugha ya Kiswahili ni muhimu katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki kwa kuwa unatuunganisha sanjari na Makabila yote yaliyopo kwenye ukanda huu, kwa hiyo ndio maana nasema lugha ya Kiswahili ni lugha muhimu kuitangaza na kukuza pia ”, ameeleza Mhe. Mchengerwa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa SAFAL Group, Anders Lindgren ameshukuru kwa ujio wa wadau wote na kusisitiza kuwa Kampuni yao itaendelea kuwekeza katika jamii ikitambua umuhimu wa jamii zinazotuzunguka.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Washindi wa 2021, Mshindi wa tuzo ya Riwaya, Halfani Sudy alitoa shukrani za dhati kwa waandaaji na wadhamini wa tuzo akisema”, Tuzo hizo zimetupa jukwaa la kukutana na wadau muhimu na kufunguka kiuchumi, hii ikiwa ni juu ya zawadi ya fedha taslim kama washindi”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi tuzo mshindi wa kwanza wa Riwaya, Khalfan Sudy (kushoto) katika hafla ya utwaji wa tuzo za Kiswahili ya Mabati - Cornell ya Fasihi ya Afrika iliyoandaliwa na Kampuni ya Mabati ya ALAF, Tanzania hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabati ya ALAF Tanzania, Ashish Mistry, katika hafla ya utwaji wa tuzo za Kiswahili ya Mabati – Cornell ya Fasihi ya Afrika iliyoandaliwa na Kampuni ya Mabati ya ALAF Tanzania tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...