Naibu waziri wa Madini Dkt.Stephen Kiruswa amewataka wachimbaji wa madini nchini kuhakikisha,kuwa wanatoa ushirikiano wakati zoezi la sensa ya watu na makazi itakapokuwa inafanyika hapa nchini.

Dkt.Kiruswa alisema kuwa Wizara ya Madini imeandaa dodoso ambalo ni maalum kwa ajili ya sekta hiyo pindi ambapo,alisema lengo ni kuendelea kuboresha sekta hiyo ili iendelee kunufaisha taifa,wachimbaji na wafanyabiashara.

Naibu waziri ameyasema hayo wakati akifungua semina ya siku moja ya sensa kwa viongozi wa madhehebu mbali mbali na Viongozi wa Mila laigwanan na Washili,wakati akimuwakilisha Waziri wa Madini Dotto Biteko,iliyoandaliwa na Taasisi ya Dini ya Twariqatul Qadiraya  Jailaniya  Araza Quiya ambapo alisema kuwa sense ni muhimu katika uchumi wa nchi kwa kuwa inaiwezesha serikali kupata taarifa sahihi na za msingi.

“Ndugu  zangu  viongozi wa dini na mila sensa hufanyika kila baada ya miaka 10 ,ambapo inatusaidia serikali kutambua ina watu wangapi?hali zao zipoje?na inawezaje kupanga mipango ya maendeleo pamoja na dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025.”alisema dkt.Kiruswa

 Aidha aliongeza kuwa matokeo ya sensa  huzisadia mamlaka katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo na takwimu zinainesha kuwa kuwa mwaka 2012, idadi ya watu ilikuwa milioni 44.9,kwamba wanaume walikuwa milioni 21.8,sawa na asilimia 48.9 na wanawake walikuwa milioni 23 sawa na asilimia 51.3.

Nae msemaji wa Taasisi ya Twariqatul Qadiraya  Jailaniya  Araza Quiya bw.Haruna Hussein alimpongeza Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuchapa kazi kwa bidii huku wakimuomba endelee kupambana ili taifa lisonge mbele.

Pia bw.Haruna alisema kuwa kutokana na kazi kubwa ambayo wanafanya wameamua kumpongeza Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia zawadi ya Mbuzi kwa kazi nzuri anazozifanya.

Katibu wa Taasisi ya Twariqa Tanzania bw.Yahya Athaman Mkindi alisema kuwa mara baada ya kuona kuwa kuna zoezi la kuhesabu watu,walifikiria kuisaidia serikali kwa  kuratibu Viongozi wa dini na mila ili basi waweze kupatiwa elimu na kwenda kuelimisha umma katika maeneo hayo.

Mratibu wa sensa  mkoa wa Arusha bi.Leokadia Atanas aliwataka viongozi wa dini kwenda kuwa mabalozi katika maeneo yao ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa  ufanisi mnamo mwezi Agosti 2022.

Semina hiyo ya siku moja imekutanisha viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Viongozi wa dini na madhehebu mbali mbali,viongozi wa siasa na vongozi wa mila.

 Naibu w├íziri wa Madini dkt.Stephen Kiruswa akiwa katika picha ya pamoja, viongozi wa dini na Viongozi wa Mila.

Mratibu wa sensa kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha bi.Leokadia Athanus akitoa elimu kwa viongozi mbali mbali walioshiriki mafunzo hayo.
Picha ya pamoja

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...