Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Washindi
wa mwaka 2022 wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya
Afrika wanatarajia kutangazwa Alhamisi ya Januari 27, 2022 katika ukumbi
wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam, Meneja Uhusiano na Mawasiliano
wa wa ALAF Limeted, Hawa Bayumi amesema kuwa shughuli ya kutangazwa
washindi hao itahudhuriwa na wadau mbalimbali wa Fasihi na Lugha ya
Kiswahili.
“Kuna
jopo la Majaji watatu watasoma baadhi ya kazi bora zilizoshindanishww
na baadaye kutangaza Washindi wa jumla katika kila kipengele”, amesema
Bayumi.
Bayumi
amesema Tuzo ya Kiswahili ya MABATI-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika yenye
thamani ya jumla ya Dola za Marekani 15,000 hutolewa kila mwaka kwa
miswada bora, au kwa Vitabu vilivyochapishww miaka miwili kabla ya mwaka
wa kutolewa zawadi katika fani za Riwaya, Ushairi, Wasifu, na Riwaya
Picha.
“Miswada
inayoshinda huchapishwa na Shirika la Uchapishaji Vitabu la East
African Educational Publishers (EAEP), na mswada bora wa ushairi
hufasiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa Kitabu na Shirika la Africa
Poetry Book Fund”, ameeleza Bayumi
Dhumuni
la Tuzo hiyo iliyoanzushwa mwaka 2015 na Dkt. Lizzy Attree (Mkurugenzi
wa Tuzo ya Coine) na Dkt. Mukoma wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell,
Marekani) ni kuthamini Uandishi wa Lugha ya Kiafrika, kuhimiza sanaa ya
tafsiri baina ya Lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe Pia kutafsiri
maandishi ya Lugha nyingine kwa lugha za Kiafrika.
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa wa ALAF Limeted, Hawa Bayumi (wa katikati)
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kutangazwa Washindi wa mwaka
2022 wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika,
washindi hao wanatarajiwa kutangazwa Alhamisi ya Januari 27, 2022 katika
ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...