Na. John Mapepele- WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa amesema Wizara yake itahakikisha inafanya kazi kuanzia ngazi ya mitaa na vijiji ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hizo katika kipindi kifupi.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo usiku wa ( Januari 14, 2022) kuamkia leo akiwa Mgeni Rasmi kwenye fainali za mashindano ya wa sanaa ya Bongo Star Search (BSS) 2022 jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi, na Naibu Katibu Mkuu, Said Yakubu

“Tunataka tuizungumze sanaa katika kila mtaa, tutaizungumza Sanaa katika kila kata, tutaizungumza Sanaa katika kila wilaya, na tutaizungumza Sanaa katika kila mkoa, tunataka Sanaa ndiyo iwe msingi wa kuendeleza katika kulinda na kuendeleza utamaduni wa taifa letu” amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Amesema kwa Wizara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanakwenda kufanya mageuzi katika sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aidha, amesisitiza kuwa yeye ni mtu wa kasi katika utendaji na matokeo zaidi hivyo atahakikisha kuwa matokeo makubwa yanapatikana katika Wizara yake.

Mhe. Mchengerwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake. Dkt. Hassan Abbasi kuona uwezekano wa kuwaendeleza washiriki wote wa shindano hilo katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo kilicho chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ni Bryson Yohana kutoka Dar es Salaam ambapo mshindi wa pili ni Andrew Charles kutoka Mwanza na mshindi wa tatu ni Suleiya Abdi mwanadada kutoka mkoa wa Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...