Meneja wa maduka ya Rejareja Vodacom, Vanessa Mlawi (kulia) akielezea ubora wa bidhaa na huduma zinazotolewa kwenye maduka ya Vodacom yaliyotapakaa nchi nzima kwa waziri wa habari, Nape Nnauye alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo leo asubuhi



Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose, Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia mara baada ya ziara ya waziri huyo kwenye makao makuu ya ofisi za Vodacom jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Fedha Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku akielezea mbele ya waziri na watendaji wa Vodacom na TCRA namna ambavyo mpango mkakati wa fedha wa mwaka 2021-22 unavyofanya kazi



Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano na watendaji wakuu wa kampuni ya mawasiliano Vodacom pamoja na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea makampuni ya simu leo akiambatana na viongozi wa mamlaka ya mawasiliano nchini. Kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Mkurugenzi mkuu Vodacom , Sitholizwe Mdlalose na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Rosalynn Mworia




Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (katikati) akibadilishana mawazo na mwenyekiti wa bodi kampuni ya Vodacom , Jaji mstaafu Thomas Mihayo (wa pili kushoto), Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi Vodacom, Margaret Ikongo (wa pili kulia) Mkurugenzi mkuu Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Rosalynn Mworia, wakati wa ziara yake ya kutembelea makampuni ya simu leo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...