Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mahakama ya mwanzo Lugarawa halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemuhukumu Ombeni Ngwa'vi (25) kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba na miaka miwili kwa kuiba debe moja la maharage ambapo vifungo hivyo vitaenda kwa kufuatana na si sambamba.

Akisomewa shitaka hilo Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu Timoth Mwakisambwe imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya mchana ambapo alivunja nyumba ya Evaristo Mgimba kisha kuiba debe moja la maharage yenye thamani ya shilingi 30,000.

Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 294(1)(a),  258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019

.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...