BABA
mzazi wa mfanyabiashara maarufu wa Mjini Babati Mkoani Manyara, Samson
Loi Mollel aliyefariki Mei 20 amezikwa jana nyumbani kwake jijini
Arusha.
Marehemu mzee
Mollel ni baba mzazi wa mfanyabiashara maarufu wa Mjini Babati, Emmanuel
Mollel wa maduka ya vifaa vya ujenzi Manuu Hardware na nyumba za kulala
wageni ya New Dream.
Marehemu
mzee Mollel ambaye alizaliwa Mei 5 mwaka 1937 katika kata ya Sokoni 2
Mkoani Arusha amebahatika kupata watoto 17 wakiume nane na wakike tisa
ila wanne wametangulia mbele ya haki.
Marehemu mzee Mollel ambaye katika kipindi cha uhai wake alijihusisha na kilimo na biashara alipata wajukuu 62 na vitukuu 25.
Akizungumza
kwenye mazishi hayo mfanyabiashara maarufu Emmanuel Mollel (Manu
Hardware) amewashukuru ndugu jamaa na marafiki waliofika kumsindikiza
marehemu baba yake kwenye safari yake ya mwisho.
"Marafiki
na jamaa zangu wengi wametoka Babati hadi huku Arusha kushiriki mazishi
ya, baba yetu tunawashukuru sana kuja kutufariji, Baba yetu amevipiga
vita vilivyo vizuri mwendo ameumaliza imani ameilinda" amesema.
Amesema siyo rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja kwa kadri ya uhusika wake, anawaomba wote kwa pamoja wapokee shukuranj za dhati.
"Baba
yetu alikuwa mpenda watu, mcheshi na alitoa ushirikiano na jamii,
hakuwahi kumbagua mtu yeyote yule na aliwapenda watu wa nyumba yake,
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe," amesema.
Mbunge
wa viti maalum Vijana Taifa kupitia mkoa wa Manyara, Asia Halamga
akizungumza kwenye mazishi hayo amesema amewawakilisha wabunge wa mkoa
wa Manyara ambao hivi sasa wapo
Bungeni jijini Dodoma.
Bungeni jijini Dodoma.
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Hiiti amesema kwenye
mazishi yao wamewawakilisha madiwani wenzao akiwa na Diwani wa kata ya
Bagara Yona Sulle.
Kada
maarufu wa CCM Mjini Babati Cosmas Masauda amesema mfanyabiashara Manuu
Hardware ni mtu wa kujitoa kwenye matukio mbalimbali ya watu ndiyo
sababu amesindikizwa na watu wengi kutoka Mkoani Manyara.
Mdau
wa maendeleo wa Mjini Babati, Emmanuel Khambay amesema wameshiriki
kumfariji mdau mwenzao Manuu Hardware kwenye mazishi ya baba yake
marehemu mzee Mollel.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...