BODI ya Filamu Tanzania katika jitihada za kuhakikisha kuwa Wadau wa Filamu wanaongeza ubora katika utayarishaji wa Filamu zinazokubalika Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza masoko ya Filamu imezindua mafunzo kwa Wadau wa Filamu jijini Dodoma .

Akifungua mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Bodi Dkt. Kiagho Kilonzo amewataka Wadau wa Filamu kutumia fursa hiyo kujiongezea maarifa mbalimbali kupitia mada zitakazotolewa sambamba na mafunzo kwa vitendo yanayoendelea. Akieleza ni matarajio ya Bodi kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika kuwaanda wataalamu watakatoa Filamu bora zitakazochangia kuongeza ajira na kipato kwa Wadau wa Filamu na Uchumi.

Aidha, ilibainishwa kuwa baadhi ya mada zitakazokuwa katika mafunzo hayo ni pamoja na masuala ya uandishi wa miswaada, upigaji picha, uhariri na uongozaji wa Filamu.

Wawezeshaji katika Mafunzo hayo ni pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Haki na Maendeleo ya Wasanii kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Asha Salim Mshana, Bw. Sikalion Rwabona kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na Bw. Ally Makata kutoka Bodi ya Filamu.

Washiriki wa Mafunzo hayo ni Wadau mbalimbali wa Filamu wa Jiji la Dodoma wakiwemo Wapiga Picha, Waigizaji, Wahariri, Waongozaji, Waandishi wa Miswaada. Mafunzo hayo yanatarajia kufikia Tamati Mei 30, 2022 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Haki na Maendeleo ya Wasanii kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Asha Salim Mshana akisisitiza mbinu bora za kuzingatia katika utayarishaji wa Filamu wakati wa Mafunzo ya Filamu.


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo akifungua Mafunzo ya Filamu kwa Wadau wa Filamu yaliyoandaliwa na Bodi kwa lengo la kuwajengea uwezo Wadau, Jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...