Na.Khadija Seif, Michuzi TV

UONGOZI wa Wasafi Media wameitambulisha rasmi Kampeni ya Mchezo wa ubashiri inayokwenda Kwa jina la "Chota Mihela'' kama sehemu ya kugawa pesa Kwa wasikilizaji na watazamaji wa wasafi.

Akizungumza mara baada kutambulisha Kampeni hiyo Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu Cha Wasafi Media Lily Ommy amesema Kampeni hiyo imekidhi vigezo na imepewa dhamana na bodi ya Michezo ya ubashiri Huku watu chini ya Miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki na atakaeibuka Mshindi pesa zake atatumiwa kwenye namba aliyoitumia kutupia ubashiri wake.

"Vipindi vyote kutoka wasafi tv na wasafi redio vitakua vinatoa pesa kupitia Kampeni ya "Chota mihela" Kwa Kila siku na Kila lisaa milioni 1 Kwa washindi 10 na milioni 5 Kwa Mshindi 1."

Kwa upande wake Mtangazaji wa kipindi cha 'Masham sham' katika redio ya wasafi fm Khadija Shaibu maarufu kama 'Dida Shaibu' amesema Kampeni hiyo
itaenda kusaidia wamama Wenye uhitaji hasa Wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wamama ntilie ,wauza vitumbua kupitia Kampeni hii inaenda kukupa mtaji wa kibiashara kwani Kipindi cha Masham sham kimekua msaada wa kutoa mitaji Kwa wakina mama hivyo itakua msaada sana Kwenye hilo.

Hata hivyo Kampeni hiyo mara baada ya kutambulishwa wasikilizaji walipewa nafasi ya kufanya ubashiri wao katika kuizindua Kampeni ya "Chota Mihela''
na hatimae Msikilizaji kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Prince Heri Mwanga akaibuka Mshindi wa shilingi milioni 5 .

:Mtangazaji wa kipindi cha 'Masham sham' Khadija Shaibu maarufu kama "Dida" akizungumza mara baada ya kutambulishwa Kwa Kampeni ya "Chota mihela" Kwa ajili ya wasikilizaji wa wasafi Media iliyofanyika jijini Dar es salaam
Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu Lily Ommy akiwa na Mtangazaji wa kipindi cha Mgahawani 'Baba levo' wakiwa wameshika hati ya Mshindi wa kwanza wa Kampeni ya "Chota Mihela'' Prince Heri kutoka Mkoa wa Kilimanjaro ambae aliibuka na ushindi wa Shilingi milioni 5 uzinduzi ulivofanyika jijini Dar es salaam.
:Mkurugenzi wa vipindi wa wasafi Media Nelson Kissanga akitambulisha wafanyakazi wa uongozi wa wasafi Media na mchakato mzima wa uzinduzi wa "Kampeni ya"Chota Mihela'' jijini Dar es salaam
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...