Bodi
ya watalaamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB), imebaini bado kuna waajiri
wanaoajili watu kufanya kazi za ununuzi na ugavi bila usajili wa Bodi
hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Watalaamu wa
ununuzi na ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa kwenye taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya
Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) zimeonyesha ukiukwajili wa Sheria kwa
Kitengo cha Ununuzi kuwa na Wakuu wa Vitengo wasio na sifa za Kitaaluma.
Pia
Mbanyi amesema taarifa hizo zimebaini mapungufu makubwa kwenye ukidhi
wa Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake na kupelekea hasara kwa
Serikali.
"Kifungu
cha 11 kimeweka sharti la ulazima kwa kila anayefanya kazi za ununuzi
na ugavi awe amesajiliwa na PSPTB. Kifungu cha 46 kimezuia kuajiri au
kufanya kazi za ununuzi na ugavi kwa mtu yeyote ambaye hajasajiliwa na
PSPTB. Na kukiuka Kifungu tajwa ni kosa la jinai na adhabu yake ni
kifungo kisichozidi miaka miwili Jela, au faini isiyozidi milioni mbili
au vyote kwa pamoja." Alisema Mbanyi
Mbanyi amesisitiza kuwa PSPTB
inawataka wataalam wote wanaofanya kazi kwenye kitengo cha ununuzi na
ugavi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao
kwa mujibu wa PSPTB Code of Ethics and Conduct GN. 365/2009 inayowataka
wataalamu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo
ili kutoa huduma yenye kukizi viwango.
Pia
Mbanyi ametoa wito kuwa PSPTB inawaagiza watalamu wa ununuzi
na ugavi wa sekta binafsi na umma kufanya kazi kwa weledi na kutoa
ushauri kwa umakini bila hofu ili kupata thamani ya fedha.
"PSPTB
inawataka waajiri wote kuwaondoa kwenye kitengo cha ununuzi na ugavi
maafisa wote wasio na sifa za Kitaalam kwa mujibu wa muongozo wa usajili
wa PSPTB na muondo wa utumishi wa kada zilizopo chini ya Wizara ya
Fedha na Mipango, Waraka No. 03 wa mwaka 2015." Alisema Mbanyi
PSPTB
inawataka waajiri kuhakikisha wakuu wa vitengo vya ununuzi na ugavi
wana sifa ya usajili wa ngazi ya juu (“authorized category”).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Watalaamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB), Godfred
Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwepo wa wafanyakazi
wanaofanya kazi bila kusajiliwa na Bodi hiyo uliofanyika katika ofisi
zake zilizopo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma (
PSPTB), Shamim Mdee .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...