Na.Khadija Seif, Michuzi TV


BAADHI ya  wafanaybiashara wa Halmashauri ya Manispaa ya ubungo wamejitolea kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji wa Kodi Kwa hiari ili kusaidia kuboreshwa Kwa Miundombinu na Miradi mbalimbali kwa kutumia Mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akizungumza mara baada ya kufungua semina ya ulipaji kodi kwa hiari katika  Afisa biashara wa Manispaa ya ubungo Prisca Mjema amesema Kila Mfanyabiashara ni muhimu kuhakikisha anajenga uelewa wa kulipa Kodi kwa hiari bila shurti.

Hata hivyo Mjema Amekiri kuwepo Kwa changamoto ya kusuasua kwa ulipaji wa Kodi Kwa hiari na kubaini kuwa Wafanyabiashara wengi wemekosa Elimu ya kutosha kuhusu kulipa Kodi, tozo pamoja na ushuru Kwa biashara ndogondogo hivyo wameona Kuna umuhimu Kampeni hiyo kutumia Mitandao ya kijamii pamoja na kukutanisha Wafanyabiashara kuwapatia semina.

" Tumeona ni vyema kushirikishana katika hili na kuwa mabalozi lengo la kutoa Elimu ya ulipaji Kwa kutumia Mitandao ya kijamii kama Instagram ,Facebook na Twitter kutokana na kuwepo Kwa utawandazi hivyo itasaidia na kurahisisha kusaambaa Kwa elimu hii Kwa haraka zaidi."

Mjema ametoa wito Kwa Wafanyabiashara kuhakikisha wanalipia leseni za biashara Kwa wakati ndani ya siku 21 Ili kuepuka usumbufu wa fidia.

Nae Mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi Fransic Woiso amebaini kuwepo Kwa kadhia ya viongozi kutoka Manispaa kutoweka Mazingira rafiki Kwa Wafanyabiashara na kuwajengea hofu kutokana na wakifika maeneo ya Biashara wanawahi kutekeleza amri Yao pasipo kumpa elimu Mfanyabiashara huyo Kwa jinsi gani Kodi yake itaweza kunufaisha Halmashauri yake kimaendeleo.

"Nikiri kumekuwepo Kwa Kadhia ya kutokuwepo Mazingira rafiki kati ya kiongozi wa Halmashauri anapofika eneo la biashara na Mfanyabiashara mwenyewe ni Miongoni mwa vitu vinavosababisha kutolipwa Kwa wakati Kodi ya Mapato."

Pia Woiso amehaidi kuwa Balozi wa mfano kuhakikisha anawapatia Wafanyabiashara Elimu ya ulipaji kodi kwa hiari kuanzia kwenye magroup ya Mitandao ya kijamii Kwa Wafanyabiashara wote.
Afisa Biashara wa Halmashauri ya Manispaa ya ubungo Prisca Mjema akizungumza na Wafanyabiashara mara baada ya kufungua semina ya siku 3 jijini Dar es salaam yenye lengo la kutoa Elimu kwa ulipaji kodi kwa hiari Kwa Wafanyabiashara na kukusanya changamoto za Wafanyabiashara hao
Wafanyabiashara wakiwa pamoja na viongozi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya ubungo ikiongoza na Afisa Biashara prisca Mjema pamoja na Mhasibu wa Halmashauri hiyo Adam wakati wa kumaliza semina Wafanyabiashara kupitia Kampeni kutoa Elimu ya ulipaji kodi kwa hiari
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...