Benki ya NMB imekuja na bima ya mali ambayo ni maalum kwa ajili ya kulinda mali zako dhidi ya majanga yatakayotokea ikiwa ni pamoja na jengo na vitu vya ndani ikiwemo samani.

Bima hii inamkinga mteja dhidi ya majanga yatokanayo na moto,radi, tetemeko la ardhi,  mlipuko wa Volkano , mafuriko, maandamano na migomo yasiyo ya kisiasa, kupasuka au kufurika kwa tanki la maji, bomba au vifaa vyake.

Aidha, wizi wa kutumia nguvu za kuingia kwenye jengo na kuiba, madhara kwa majengo kutokana na chombo cha moto au wanyama wasiomilikiwa na mwenye bima.

Kwa upande wa viwango vya bima, vinatolewa kulingana na thamani iliyowekwa katika bima, inategemea na gharama elekezi inayotolewa na mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA).

 Mfano;

Thamani ya nyumba(Tshs)

Tshs. 100,000,000

Agizo la kiwango(%) cha chini 2018 ni 0.15

0.15

Kiwango bila VAT

Tshs. 150,000

Pamoja na VAT 18%(Tshs)

Tshs. 27,000

Kiwango(Pamoja na VAT)

Tshs. 177,000

 

Unachohitaji;

ü  Umiliki na Kitambulisho halali

ü  Fomu ya gharama na viwango

ü  Orodha ya vitu na gharama zake

ü  Thamani ya mali

Janga litakapotokea, toa taarifa za madai katika tawi lolote la NMB karibu yako piga simu namba 0800 002 002 bure!

Pia, ambatana na ripoti ya polisi katika masuala ya wizi(loss report) au ripoti ya jeshi la kuzima moto na gharama za marejesho/marekebisho.

Umebima-SiNgumuKihivyo!


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...