Na.Khadija Seif, Michuzitv

Waziri Wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Dkt.Stergomena Tax anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi katika shindano la mchezo wa Gofu kwa upande wa Wanawake "Lugalo Ladies Open 2022" litakalofanyika mei 21 na 22 katika klabu ya Lugalo Gofu jijini Dar es salaam.

Shindano hilo likiwa na lengo la kuenzi siku ya mama Duniani pamoja na kuunga mkono juhudi za Mh Rais Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii wa ndani na kukuza michezo nchini.

Akizungumza wakati wakutambulisha shindano hilo, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema, wanawake wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa na kuhakikisha wanautangaza mchezo huo na kurudi na Ushindi Nchini.

Kwa upande Wa Nahodha wa wanawake wa Klabu hiyo Hawa Wanyeche, amesema shindano hilo litakuwa ni la stroke play na litahusisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali nchi Pamoja na wachezaji Kutoka ya Nchini Uganda.

Mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya SBC Tanzania Limited, Meneja Uhusiano Doris Malulu,Amesema wanafarijika kuwa miongoni wa wadhamini wa mashindano hayo na ameahidi watendelea kudhamini mashindano mengine ya mchezo huo.

Shindano hilo la "Lugalo Ladies Open 2022" linatarajiwa kufanyika mei 21 hadi 22 mwaka huu likihusisha klabu mbalimbali za Mchezo wa Gofu Ikiwemo,wenyeji Lugalo Gofu, Dar Gymkhana,Morogoro Gymkhana,Arusha Gymkhana,kill Gofu,Tpc Moshi Pamoja na wachezaji Kutoka nchi jirani ya Uganda.


Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo gofu Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo akizungumza na waandishi Wahabari mara baada ya kutangaza Shindano la " Lugalo ladies open " linalotarajiwa kuanza mei 21 mwaka huu katika viwanja vya Klabu ya jeshi lugalo gofu jijini Dar es salaam

Nahodha wa wanawake wa Klabu ya lugalo gofu  Hawa wanyeche  akitolea ufafanuzi Klabu zitakazoshiriki ni litahusisha  vilabu mbalimbali pamoja na wachezaji kutoka nchini uganda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...