Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakati kasi ya kilimo cha zao la matunda ya Parachichi ikiongezeka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hivi sasa,Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba amewataka wakulima wilayani Wanging’ombe hususani vijana kuendelea kulima zao hilo kwa tija bila kusahau kujenga utamaduni wakujiwekea akiba kwenye mifuko ya hifa ya jamii itakayowasaidia wakati wa uzeeni.

Ameyasema hayo wakati alipofungua mkutano wa wadau wa zao la Parachichi wilayani Wanging’ombe kwa malengo mbali mbali ikiwemo pia kuwahamasisha wakulima kuchangamkia fursa za kujiunga na mifuko ya jamii pamoja na kuzitafutia ufumbuzi changomoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa zao hilo ikiwemo upande wa masoko.

“Sasa hivi tuna nguvu lakini baada ya muda uzee umeingia,sasa uzee ukiingia hii mifuko ya jamii inakuwepo kwa ajili ya kukusaidia tusije tukalidharau hilo”alisema Kindamba

Meneja wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mkoa wa Njombe Bwana Juma Mwita ametoa rai kwa wakulima kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ili kupata msaada wakati wa uzee kwa sababu uzee ni janga la uzeeni.

“Uzee ni janga,unaposhindwa kuzalisha na kujihudumia ni janga kwa hiyo kuna faida pia kwa mkulima kujiunga ili anaposhindwa kuzalisha anakuwa na uhakika wa kuhudumiwa na mfuko wa hifadhi”alisema Mwita

Zao la parachichi ambalo ni dhahabu ya kijani hivi sasa mkoani Njombe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Bi. Maryam Mhaji anaelezea nia yao ya kuwakutanisha wadau wa zao hilo.

“Kuna changamoto sana ya masoko tukaona tuwashirikishe taasisi ambazo serikali imezipa uwezo wa kuzitafutia masoko kwasababu kuna wanachi wengi wanatapeliwa”alisema Bi. Maryam Mhaji

Baadhi wakulima wa zao la parachichi walioshiriki mkutano huo, wakiwemo wanunuzi,wasambazaji wa pembejeo wamesema shauku yao kubwa ni kuona mkulima ananufaika na kilimo hicho.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akizungumza na wadau wa kilimo cha Parachichi huku pia akiagiza wafanyabiashara na makampuni yanayodaiwa na wakulima kulipa mdaeni yao ili kumsaidia mkulima.
Baadhi ya wanunuzi wa matunda ya parachichi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe wakati wa mkutano wa wadau wa kilimo hicho.

Meneja wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mkoa wa Njombe Bwana Juma Mwita akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wadau wa kilimo cha Parachichi kumalizika wilayani Wanging’ombe




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...