Na.Khadija Seif,Michuzi TV

BENDI tano zinatarajia kuumana katika jukwaa moja pamoja na kutoa burudani kibao katika tamasha la ‘Usiku wa Wafia Dansi’ litakalofanyika Jumamosi katika Ukumbi wa Gwambina jijini Dar es Salaam.


Tamasha hilo litashirikisha bendi Msondo Ngoma Music Band, Bogoss Music chini ya Nyoshi el Sadaat na Mapacha Music Band ya Jose Mara zote zinatokea Dar es Salaam huku bendi mbili kutoka nje ya Dar es Salaam ambazo ni Waluguru Original ya Morogoro na Mjengoni Classic ya Arusha.

Akizungumza na waandishi wahabari Mratibu wa tamasha hilo Bernard James kutoka Cheza Kidansi Entertainment ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo amesema maandalizi yamekamilika kwa asiilia kubwa.

“Tunashukuru tamasha hili limeanzisha safari nyingine kwa timu hizi, kwani bendi ya Mjengoni Classic na Waluguru Originali wamepata mualiko katika kumbi mbalimbali kwa ajli ya kutoa shoo,” alisema James.

Mratibu huyo ameeleza kuwa wameziweka bendi chache hizo kutokana na bajeti ya fedha ilikuwepo.

“Tulitamani kuwepo na bendi zaidi ya saba ila bajeti imesababisha tuwe na bendi chache, tunahitaji kuwa na tamasha kubwa kila la muziki wa dansi hivyo tunaruhusu wadhamini kujitokeza katika kudhamini."

Licha tamasha la Wafia Dansi kutarajiwa kupambwa na nyimbo pendwa za zamani kutokea kwa kila bendi, pia itakuwa jukwaa sahihi la washiriki kutambulisha silaha zao mpya.

Gwiji wa Muziki wa dansi Mzee Hamza Kalala maarufu kama "Komandoo" amesema atahakikisha matayarisho ya jukwaa na vifaa vinakamilika na kujigamba kuwa amejipanga vizuri kutoa burudani kali katika tamasha hilo, kuimba nyimbo mpya na zamani.

Mzee Kalala awaomba watanzania na wadau wa muziki huo kujitokeza kwa wingi katika ukumbi huo wa Gwambina kushuhudia burudani kali kutoka kwa wakali hao

 


 Gwiji wa Muziki wa dansi nchini Hamza Kalala maarufu kama Komandoo akichagiza Mashabiki kujitokeza Kwa wingi katika tamasha la Msimu wa 4 wa wafia dansi linalotarajiwa kufanyika mei 28 katika ukumbi wa gwambina Jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...