Na Said Mwishehe, Michuzi TV

NAOMBA nianze kutoa salamu za unyenyekevu mkubwa kwa Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan. Mama shikamoo! Natumai unaendelea salama na majukumu ya kuliongoza Taifa letu.

Nikiri binafsi Mimi ni miongoni mwa Watanzania ambao wanavutiwa na utendaji kazi wako Rais wangu.

Huna baya, huna lawama na kubwa zaidi unajua namna ya kushughulika na changamoto zilizopo kwenye nchi yetu. Huna makuu Rais wangu, unaiongoza nchi kwa utulivu mkubwa. Na sasa nikwambie huku mtaani tunasema hivi Mama anaupiga mwingi.

Najua wapo wanaokuchukulia poa, wapo wanaonong'ona ooooh mbona mambo hayaendi, wengine utasikia wakisema eti miradi imesimama.Huwa nawaangalia halafu nasema usichokijua ni sawa na usiku wa giza nene.

Sijui wakoje wamekaa kupotosha potosha tu ukweli, lakini tunaokuelew tunaachana nao tunajua ipo siku wataungana na sisi kukubali kazi yako.

Rais wangu usihangaike na wanaobeza mafaniko ambayo tumeyapata katika kipindi chako cha mwaka mmoja madarakani. Wenye macho tunaona,wenye masikio tunasikia.

Umefanya kazi kubwa na ya kuonekana, tunaona mafanikio ya Serikali yako. Ukiona mtu anabishana na ukweli basi huyo  ana lake jambo.

Rais wangu ninachosikitika ni kwamba mengi ambayo umeyafanya wanaopaswa kusema wamekaa kimya, walio wengi wapo wapo tu yaani kama wamepigwa ganzi ya macho na masikio. Fedha zinakwenda na kisha zinapokelewa na miradi inatekelezwa basi wenye nafasi ya kuelezea mafanikio hawasemi wako kimya yaani kimya kabisa.Najiuliza Kuna nini? Nakosa jibu.

Rais wangu naamini wengi ambao umewateua kwenye nafasi unawamudu, ukipata nafasi zungumza nao, nadhani wanastahili kukumbushwa wajibu wao, wamesahau kuwa wanayo nafasi ya kuuelezea Umma yale ambayo umeyafanya katika kipindi cha mwaka mmoja .

Rais wangu nakumbuka ambavyo umekuwa ukiwaambia Watanzania hakuna mradi wowote ambao ulianzishwa kwenye Serikali ya Awamu ya Tano halafu Awamu ya Sita ambayo wewe unaiongoza isitekeleze, ukweli uliopo miradi inatekelezwa tena kwa kasi kubwa, tofauti tu ni kwamba wanaopaswa kuelezea miradi hiyo wamekaa kimya.

Rais wangu naomba nikwambie ukipata nafasi ya kuzungumza na uliowapa majukumu ya kukusaidia kwenye kutekeleza majukumu yako wakumbushe pia wawaambie maofisa habari walioko kwenye sekta za umma wasikae kimya.

Rais wangu naomba nikwambie najua pia  maofisa habari wamekuwa wakiyazungumzia yaliyofanyika lakini kasi yao ya kuzungumza imekuwa ya kusuasua. Sitaki kuamini kama kuna maelekezo kwamba wakae kimya, siamini kabisa,kweli tena.

Nachoamini wanatakiwa kukumbushwa wajibu wao.Siwachongei lakini wajitafakari,mbona  miwili nyuma hawakuwa kimya, sasa  hivi wamepatwa na nini?
 
Rais wangu naomba nitoe mfano mdogo tu wa mambo machache kati ya mengi ambayo umeyafanya katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wako, tena hapa sitaizungumzia filamu ya Royal Tour ambayo umeizindua hivi karibuni nchini Marekani na baadae Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam.

Hongera Rais  kwa kuipeleka nchi yetu kwenye ulimwengu wa Kimataifa, kupitia Royal Tour Tanzania yangu inatambulika na kubwa zaidi umeiambia Dunia mlima Kilimanjaro na madini ya Tanzanite ni mali ya watanzania.

Ahsante Rais Samia, umeanika kila kitu tulichonacho,hakika umefungua fursa nyingi, faida ya filamu Ile imeanza kuonekana.

Rais wangu ngoja niseme tu uliyoyafanya tena kwa uchache tu, ndani ya mwaka mmoja umepunguza gharama za matibabu ya figo kwa asilimia 66, umejenga madarasa 17000 nchi nzima, umevifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa.

Rais wangu nasema ahsante kwasababu umemaliza Ujenzi wa Daraja la Tanzanite, umepandisha  mishahara kwa Wafanyakazi kwa asilimia 23.3, umefuta  stakabadhi ghalani kwa mazao ya Pamba,dengu Choroko, Mbaazi na Ufuta.

Rais wangu katika mwaka mmoja wa uongozi wako umepandisha  bei ya mbaazi kutoka shilingi mia 300 kwa kilo hadi shilingi 3000,miezi sita ya kwanza ya Rais Samia uwekezaji ulikua kwa asilimia  400 Ukafikia USD 3BL toka USD 510M | Nikaribu mara sita zaidi ya ule wa mtangulizi wake katika kipindi kama hicho.

Rais wangu umepandisha  Bajeti ya barabara,madaraja na viwanja vya ndege inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano iliyopita. Barabara zinaendelea kujengwa. Umeongeza  bajeti kwa asilimia  230 kutoka Sh.trilioni 1.1 mwaka 2020/2021 hadi Sh.trilioni 2.34 mwaka 2021/2022 katika Mradi wa bwawa la Umeme la JNHP.

Umetoa zaidi ya Sh.bilioni  12.6 kujenga kilometa 12.6 za Lami kuzunguka eneo la Viwanda la Yaani "Ummy Mwalimu Industral Park -Kahama Shinyanga. Umerejesha haki za Binadamu na utawala bora.

Rais wangu umerejesha  ushirikiano na kati ya Sekta Binafsi na Serikali, umepunguza utegemezi wa misaada na mikopo nafuu toka kwa wahisani ( donor country ) kutoka 8.2% ya bajeti ya FY2020|21 hadi 8.1% FY 2021|22 kwa  Serikali ya awamu ya sita imepunguza asilimia za misaada kutoka nje katika bajeti ya maendeleo.

Katika kipindi Cha mwaka mmoja Rais wangu umelipa madeni yenye thamani ya jumla ya zaidi ya Sh.trilioni 11.17623 yaliyoachwa na mtangulizi wako.Umetoa Jumla ya fedha kiasi cha Sh Bilioni  2.17 ili kuwalipa watoa huduma mbalimbali waliokuwa wanaidai Serikali kutoka katika Wizara mbalimbali.

Rais wangu umetoa jumla ya fedha kiasi cha Sh.bilioni 70.49 kwaajili ya kuwalipa Wazabuni  mbalimbali waliotoa bidhaa na huduma kwa Serikali yetu.Umetoa jumla ya fedha kiasi cha Sh.bilioni 264.23 kwaajili ya kuwalipa wakandarasi wetu mbalimbali wa nje na ndani waliokuwa wanaidai Serikali.

Rais wangu umetoa jumla ya fedha kiasi cha TZS 111.41BL ili kuwalipa watumishi wa Serikali wanaoidai Serikali. Malimbikizo pamoja na viinua mgongo kwa watumishi mbalimbali.

Serikali  imenunua Jumla ya ambulance mpya 395 na magari mapya 214 kwa ajili ya chanjo kwa mpigo kitu ambacho hakijawahi kufanyika tangu tuwe huru kama Taifa.

Rais wangu hata akiba ya fedha zetu za Akiba  kigeni Imeongezeka kwa TZS 2.3T sasa imefikia $5.8b toka $4.8b mwezi March 2021 | Pesa hii inaweza kulisha Watanzania wote kwa miezi mitatu mfululizo yaani Wale walale tu.

Pia sitaki kusahau Rais wangu umeruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurejea shuleni.Umetoa Sh.bilioni  520 za maji Arusha ikiwa ni zaidi ya asilimia 80 ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka.​ mradi mkubwa wa maji kwa kanda ya Kaskazini.

Rais wangu umeidhinisha Mradi wa Gesi asilia. Mradi  huu utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu 15 na ajira ya muda elfu 5 na kuzalisha jumla ya tani 10M za LNG kwa mwaka, utaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa nne Africa wa Gesi asilia na kuingizia nchi fedha za kigeni zaidi ya $5.5BL au Tshs 13trilion kwa mwaka kwa kuuza hiyo tani 10 kwa bei ya $11 kwa mmbtu, Pesa hii ni sawa na 100% ya bajeti nzima ya "Maendeleo" ya nchi kwa mwaka mmoja wa Fedha.

 Umetoa Sh.bilioni 35  kujenga uwanja wa ndege wa Musoma Airport. Umeweka historia kwa kujenga madarasa mapya manne ( 4 ) katika kila ilipo shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima | haijawahi kutoka Watoto wote 1M wa kidato cha kwanza nchi nzima kuanza shule siku moja.

Rais kwa upendo wako mkubwa kwa Watanzania umetoa  ruzuku ya Sh. bilioni 100 kunusuru kupanda kwa bei ya mafuta. Kutokana na mgogoro wa Urusi na Ukraine.Umetengeneza mfuko maalum wa ruzuku kwa ajili ya mbolea kurahisisha bei ya mbole kuwa chini na nafuu kwa wakulima wote.

Hakika Rais wangu umefanya mambo mengi kwenye nchii, sitaki kuzungumza wale ambao umewatoa jela ambako walifungwa kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu, nataka nieleze tu katika kipindi chako cha mwaka mmoja kupitia fedha za UVIKO-19 Kuna miradi inaendelea kutekelezwa, mingi sana.Kwa mfano nilibahatika kuitembelea maji vijijini inayotekelezwa na RUWASA kupitia fedha hizo iko lundooo, wananchi huko vijijini ni kicheko tu, hongera Rais wangu.

Pamoja na yoooote hayo Rais wangu nashangaa kuona wanaostahili kusema hawasemi, wanasubiri useme wewe mwenyewe.Mengi yamefanyika lakini yanayosemwa  ni machache.Hapa juzi kati  nimemsikia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka akitoa maelekezo kwa wakuu wa Wilaya,wakuu wa mikoa na wakurugenzi kuisemea miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.Akasema wengi wako kimya.Nadhani nao wajitafakari.Wanaosema wapo lakini wanahesabika.

Rais wangu shaka ambayo Shaka ameionesha dhidi ya wateule kukaa kimya nadhan kuna haja ya kufanya jambo.Shaka alishasema kuhusu wateule kukaa kimya.

Rais wangu kuna jambo nilitaka kusahau kukwambia serikali itusaidie kwenye kudhibiti mfumu wa bei kwani umekuwa ukiongozeka siku hadi siku. Kuna wakati huwa natamani Serikali iangalie utaratibu wa kuwa na bei elekezi katika baadhi ya bidhaa na vyakula .Kwa mfano kupitia watalaamu wanaweza kujua kabisa bei ya unga bei elekezi , bei elekezi lwenye mchele, sukari,mafuta ya kula na aina bidhaa nyingine. Rais kwenye hili nimesema tu , kama nimewaza vizuri itakuwa poa na kama nimekosea naomba msamaha.

Rais wangu kwenye suala la uchaguzi mkuu mwaka 2025 naomba nikuhakikishie mimi na Watanzania wengine tuko pamoja na wewe, hatutarudi nyuma hata kidogo. Najua wapo baadhi ya wanasiasa wanatengeneza mazingira kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kutaka nafasi ya Urais mwaka 2025, niwaambie ukweli wenye malengo hayo  wanajisumbua, sisi ni wewe tu.

Rais wangu ndani ya mwaka mmoja umefanya makubwa hivi tunakuachaje? Mwaka 2025 hatuna mwingine ni Rais Samia tu. Watakaonuna na wanune ,ndio mshasema na uzuri tuko wengi kuliko hao wenye vijiba vya roho.

 Rais wangu nakumbuka wakati fulani uliwahi kusema wale ambao hivi sasa badala ya kuwatumikia Watanzania wanawaza urais mwaka 2025 utawaondoa kwenye baraza la mawaziri, hivi ulishawaondoa wote au bado wapo? Kwa akili yangu ndogo naona kama bado wapo vile lakini najua unavyo vyombo ambavyo kwenye hili watakuwa taarifa sahihi, wapo au hawapo.

Rais wangu naomba nihitimishe kwa kueleza hivi kwa kutumia vyombo vyako unayo nafasi ya kuangalia nani ni nani na anafanya nini kwa ajili ya nani. Utawajua tu walio wako na wasio wako.Natamani  kuona unachosema ndicho kinachotelezwa, unachoelekeza ndicho kinachofanyiwa kazi.Halafu nilitaka kusahau ahadi yako yenye tumaini kwa Wamachinga imewavutia wengi.

Rais wangu hakika umefanya mambo makubwa, nachoweza kukifanya ni kukuombea Afya njema na maisha marefu, Mungu azidi kukutia nguvu,hekima,busara na maarifa.Rais wangu ninachoweza kuhitimisha nacho ni hivi AHSANTE KWA ULIYOTUFANYIA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA NA KUBWA ZAIDI KAZI IENDELEE.

SIMU 0713833822

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...