Waziri
wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Bi.
Colette Selman, Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa linaloshughuka na
masuala ya Chanjo (GAVI).
Mazungumzo
hayo yamefanyika tarehe 25 Mei, 2022, katika Makao Makuu ya Shirika
hilo Geneva Uswisi wakati wa kikao cha 75 cha Shirika la Afya Duniani.
Waziri
Ummy amelishukuru Shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania
katika kutoa huduma ya chanjo za watoto chini ya miaka mitano.
Waziri
Ummy amesema Chanjo hizo ambazo zinawakinga watoto chini ya miaka
mitano dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo na kuongeza
kuwa Tanzania imejipanga kuwafikia watoto wote ili kuwakinga na magonjwa
hayo.
Katika
kikao hicho Waziri Ummy ameishukuru pia GAVI kuiwezesha Tanzania kupata
chanjo za UVIKO-19 zipatazo milioni 11.2 ambazo zimewezesha uchanjaji
hadi sasa kufikia asilimia 15 kati ya asilimia 70 ya kundi lililolengwa.
Waziri
Ummy ametaja changamoto ya kasi ndogo ya kuchanja ni kutokana na
kuwepo kwa imani potofu kwa baadhi ya wananchi kuhusiana na chanjo ya
UVIKO-19 pamoja na wananchi kupendelea kuchanjwa majumbani au maeneo
wanayofanyia kazi ambayo jambo ambalo ni gharama katika utekelezaji
wake.
Kwa
upande wake Bi. Collete amemshukuru Waziri Ummy kwa kumtembelea na
kujadili jinsi ya kushirikiana katika kuimarisha huduma za chanjo
Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...