Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Jumla ya watoto 256,186 sawa na asilimia 127 walio chini ya miaka mitano mkoani Pwani, wamefikiwa kwenye Kampeni ya chanjo ya matone (POLIO) inayosaidia kujenga Kinga na kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.

Lengo la mkoa ilikuwa ni kufikia watoto 200,967 hivyo kuwa na ongezeko kwenye malengo yao kwa kuwafikia watoto 55,222.

Mratibu wa chanjo Mkoani Pwani,Abbas Hincha alieleza ,zoezi limekamilika lakini vituo ambavyo vipo chini ya malengo yaliyotakiwa vinaendelea na kutoa chanjo katika maeneo Yao.

";Kampeni hii imefanyika ,kufuatia february17 mwaka huu nchi ya Malawi kutoa tamko la kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo , baada ya mtoto mmoja kutoka Mji Mkuu wa Lilongwe kuthibitika kuwa na ugonjwa huo."alifafanua Hincha.

Hata hivyo ,alisema kampeni hiyo,imefanyika nyumba kwa nyumba na katika vituo vya afya, kuanzia Mei 18 hadi Mei 21 ndani ya mkoa huo.

Alibainisha, watoto chini ya miaka mitano wamepata chanjo hii bila kujali kama walishapata chanjo katika ratiba zao za kawaida ya chanjo.

Aliitaka ,jamii itambue usalama wa chanjo hiyo , kwani Ni Kama chanjo nyingine.

Vilevile Hincha alisema kuwa, ugonjwa huo hauna tiba ila hukingwa na chanjo ya Polio ambayo ipo katika mfumo wa matone .

Hincha alisema, chanjo ni ileile inayotumika miaka yote lengo ni kuongeza kinga , kuzuia mlipuko na kudhibiti watoto wasipatwe na virusi vya ugonjwa huo.

Alieleza , kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata mgonjwa wa Polio Julai 1996 hivyo kampeni hii inatarajiwa kufanyika katika nchi zinazopakana na Malawi ikiwemo Zambia,Msumbuji, na Zimbabwe .

Ugonjwa wa polio unasababishwa na kirusi cha polio ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu alieathirika kwenda kwa mwingine kwa kunywa au kula chakula ama kinywaji kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya ugonjwa wa polio.Virusi vya polio huzaliana katika utumbo na huweza kuathiri mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa viungo ndani ya masaa machache hata kupelekea kifo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...