Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui(kulia)akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano maalum na waandishi hao kuzungumzia msafara wa wafanyabiashara kutoka nchini ufaransa waliofika Tanzania kufanya uwekezaji.(kushoto) ni kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa.



Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (wa nne kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara hao walipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawamo pichani) katika makazi yake Mei 17, 2022 Jijini Dar es Salaam.


Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Iku Kassege (kushoto) akiwa na Baadhi ya watumishi wa Ubalozi huo wakifuatilia hotuba ya Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui katika mkutano huo.

Kiongozi wa wafanyabiashara kutoka Ufaransa G'erard Wolf (katikati) akielezea mambo mbalimbali ambayo wafanyabiashara hao watakwenda kuyafanyiakazi katika uwekezaji wao hapa Tanzania. (kushoto), ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania 
Nabil Hajlaoui na (kulia) ni Pedro Novo kutoka katika jopo la wafanyabiashara kutoka Ufaransa




Baadhi ya waaandishi kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari wakifualia mkutano.





Na Said Mwishehe, Michuzi. TV 

KATIKA kuitikia mwito wa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais samia Suluhu Hasssan, nchi ya Ufaransa imesema kupitia makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya umma na binafsi ya Ufaransa kwa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo uwekezaji wao utaffikia hadi dola bilioni 4.2. 

Kwa hivyo Ufaransa itajiweka kama mwekezaji wa kwanza kabisa wa Ulaya nchini na mshirika wa kukumbukwa katika utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kufikia malengo ya nchi ya kisasana ya viwanda. Akizungumza mbele ya waandishi habari Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akiwa na wawakilishi wa kampuni 40 kutoka kwenye nchi yake ambao wako nchini Tanzania kuangalia fursa za uwekezaji ujumbe wa wakikilishi hao wamepata nafasi ya kukutana na Rais Samia, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Akifafanua zaidi Balozi Nabil Hajlaoui amesema kuanzia Mei 16 hadi 18 mwaka huu kampuni hizo 40 zikiongozwa na na mashirika ya umma na binafsi ya Ufaransa (Bpifrance, Business France na MEDEF International), wataalamu katika sekta za usafiri, nishati, maji safi, kilimo, chakula na afya zimekuwa zikiangalia fursa zilizoko nchini ili kukidhi mfumo wa ikolojia wa Tanzania wa umma/binafsi ili kukidhi mahitajiya soko. Amesema ujumbe wa uwakilishi wa kampuni hizo kutoka nchini Ufaransa umetokana na ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Ufaransa Februari 2022 na ziara ya Waziri wa Ufaransa anayeshughulikia Biashara ya Nje na Vivutio vya Uchumi, Franck Riester jijini Dar-es-Salaam Oktoba 2021.

 “Ziara ya ujumbe huu imechochewa na nia ya dhati ya kampuni za Ufaransa kwa Tanzania, nchi ambayo kutokana na ukuaji wake wa nguvu na utulivu wa kisiasa, inatoa matarajio makubwa ya maendeleo kwa wataalamu waUfaransa. Fursa hizi zinatia matumaini zaidi kwani nchi inajitahidi kurejesha hali ya biashara inayowafaa wawekezajiwa kigeni. “Wakati wa mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ufaransa mjini Paris Februari 14 wakatiwa ziara yake nchini Ufaransa, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza kuhusu mageuzi yake ya "biashara bora" na akakaribisha makampuni ya Ufaransa kuja nchini Tanzania,”ameeleza Balozi Nabil Hajlaoui. 

Amefafanua miezi mitatu baada ya mwaliko huo kampuni za Ufaransa ziliitikia kwa wingi mwito huo na walipata heshima ya kukutana na Rais jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumza katika maeneo mbalimbali yanayohusu fursa za uwekezaji. “Ufaransa ambayo kwa sasa inashikilia wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya, pia inakusudia kuisaidiaTanzania kuhamasisha vyombo vya ushirikiano wa Ulaya, kama vile mpango wa Global Gateway (hadi Euro bilioni 300 katika uwekezaji) ili kuipa nchi miundombinu bora naendelevu. 

“Tunachoweza kueleza kwa sasa ni kwamba idadi ya kampuni za Ufaransa nchini Tanzania imeongezeka zaidi ya mara tatu kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 (makampuni 40 mwaka 2022 ikilinganishwa na 12 mwaka 2019). Kwa mantiki hii, inadhirisha kuwa uwepo wa Wafaransa umepanuka lakini pia umetofautiana kuhusiana na kuongezeka kwa idadi ya biashara ndogo na za kati…

 “Na biashara za ukubwa wa kati zinazoungwa mkono na ofisi yakikanda ya Biashara ya Ufaransa, kuongezeka kwa kiwango cha Bpifrance nchini na kuongezeka kwa mamlaka ya Chama cha Wafanyabiashara wa Kifaransa na Watanzania, ambachosasa kina wanachama 40, yakiwemo makundi kadhaamakubwa ya kimataifa,”amesisitiza Balozi huyo. 

Ameongeza kwa hivyo kampuni za Ufaransa zitaendelea kuja Tanzania kwa lengo la kuhakikisha wanashirikiana katika mkakati wa muda mrefu na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi. “Wamethibitisha kuendelea kudumisha uhusiano huu kupitia miradi nauwekezaji wao nchini licha ya changamoto inayohusishwa najanga la Covid-19.

 “Kwa hivyo Ufaransa iko mbioni kuwa mwekezaji mkuu wa Ulaya nchini Tanzania, kwa sababu ina nia yakuongeza ushiriki wake wa moja kwa moja katika miradiya maendeleo ya nchi, hasa usambazaji na uzalishaji wanishati kupitia makampuni ya Ufaransa kama vile Engie, Total Energie na Maurel & Prom, usafiri na vifaa,”amesema. 

Ameeleza kama vile ushirikiano na Airbus na mradi wa ukarabati wa Terminal 2 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Bouygues Bâtiment International.Kampuni za Ufaransa pia yamejipanga katika maeneo mengine kama vile usafiri wa baharini (mradi wa bandari ya Bagamoyo). 

Pia sekta ya maji na usafi wa mazingira, mawasiliano ya simu (yaliyozinduliwa hivi karibuni na Eutelsat ya huduma yake yamtandao ya kasi ya satelaiti kupitia kampuni tanzu ya KonnectBroadband Tanzania) na afya (mradi wa hospitali) Dodoma; msaada kwa vituo vya saratani nchini kote).“Hivyo kupitia makubaliano ya ushirikiano katika kipindi cha miaka mitano ijayo uwekezaji wetu utakufa umefikia kiasi cha dola bilioni 4.2,”amesema Hajlaoui.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...