Na Pamela Mollel,Arusha

WADAU wa utalii kutoka nchi 38 duniani wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu-Kili Fair yanayotarajiwa kuanza Juni 3 hadi 5 mwaka huu mkoani Arusha.

Akizungumza jijini Arusha, Mkurugenzi wa Kilifair Ltd ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo, Dominic Shoo,alisema lengo la maonyesho hayo kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

Anasema mbali na nchi hizo akithibitisha ushiriki wao,pia waonyeshaji kwenye mabanda kutoka nchi 12 watashiriki.

"Royal Tour aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan imetusaidia kuitangaza nchi,hivyo Dunia inafahamu Tanzania,imetupa urahisi mkubwa sanaaa wakufanya Kilifair"anasema Shoo

Alisema onyesho hilo litakuwa la kipekee, baada ya Dunia kukumbwa na janga la Covid-19 na kutakuwa na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

"Katika maonyesho haya pia tunatarajia washiriki 380 kutoka nchi hizo na wengine kutoka nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao wametuomba tutangaze vivutio vilivyopo katika nchi hizo kama vivutio vya pamoja,"alisema.

Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Kaskazini,Dismas Prosper alisema wao pia ni miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo, wakiamini utalii ni sehemu kubwa ya uchumi Kanda ya Kaskazini.

Alisema pia katika kunyanyua sekta ya utalii pia wamefadhili Sh.milioni 59 katika maonyesho hayo ili yafane na kukidhi haja kwa wageni watakaohudhuria katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

"Sisi tumejipanga kuhudumia wageni wetu watakaokuja na waliopo kwa kutoa huduma bora ya kubadilisha fedha kwa kuweka mashine za ATM kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) na tumeboresha na kujenga mahusinao mazuri na wafanyabiashra mbalimbali wa sekta ya utalii,"alisema Prosper

"Tunahitaji kukuza sekta ya utalii nchini na Benki yetu imejikita katika kuhakikisha inasaidia Kilifear kufanikisha maonyesho ya kimataifa ya kanda hii ya Afrika Mashariki "aliongeza

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi maendeleo ya biashara Beatrice Kessy anasema maonyesho hayo yanasaidia sana kutangaza utalii wetu na fursa zilizopo


Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Dismas Prosper akikabidhi hundi ya shilingi milioni 59kwa waandaaji wa maonyesho  ya kimataifa ya Karibu Kilifair , kwaajili ya kufanikisha maonyesho hayo yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha

Kamishna Msaidizi maendeleo ya biashara Beatrice Kessy
Meneja wa benki ya NMB kanda ya kaskazini Dismas Prosper

Mkurugenzi wa KILIFAIR Dominic Shoo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maonyesho ya kimataifa ya karibu Kilifair


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...