Na Janeth Raphael
MAEFU ya wananchi wa Wilaya ya Mwanga Mkoani kilimanjaro wamejitokeza kushiriki

zoezi la msaragambo kusafisha na kuchimba msingi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa hospitali ya mpya ya kisasa Wilayani hapo

Ujenzi huo wa hospitali ya Wilaya unatarajiwa kuanza na tayari Serikali imeshatoa fedha za awamu ya kwanza shilingi bilion 1 ambapo gharama yote ya ujenzi mpaka kukamilika inakadiriwa kuwa shilingi za Kitanzanja bilioni 3.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mbunge wa jimbo la Mwanga Joseph Tadayo amesema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni moja ya ahadi ya mheshimiwa Rais wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 kutokana na Wananchi wa ukanda wa tambarare wanaokabiliwa na changamoto za huduma ya afya na kufuata hospitali ya Wilaya usangi na hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro mawenzi.

Mbunge Tadayo amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutapunguza adha kwa

wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya mbalimbali katika hospitali ya Wilaya usangi ambayo iko mlimani na kwamba wananchi wa ukanda wa tambarare wanashindwa kufika kwa urahisi.

Tadayo ameendelea kusema kuwa kukamilika hospitali hiyo kutaboresha upatikanaji wa huduma za afya ndani ya Mwanga na wilaya jirani za Same na Moshi vijijini hata kwa wasafiri kutokana na hospitali hiyo kujengwa jirani na barabara kuu iendayo Dar es salaam-Arusha.

"Hospitali hii ni yakisasa pia iko barabara kuu iendayo Dar es salaam -Arusha hivyo ni rahisi inapotokea ajali za barabarani (hatuombei hivyo) majeruhi watapatiwa huduma kwa haraka badala ya kupelekea hospitali ya rufaa mawenzi au hata hospitali ya Kanda KCMC ambapo pia ni mbali," - amesema.

Amesema mpango huu wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya katika ukanda huu wa tambarare ni mpango wa muda mrefu wa wazee wa Mwanga na baba wa Mwanga Mzee David Cleopa Msuya ambapo walikaa nakutenga eneo zaidi ya ekari 53.

"Kwa zaidi ya miaka 30 wananchi wamekuwa wakisubiri ujenzi wa hospitali hiyo ambapo Serikali ya awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya

kukamilisha ujenzi huo,"amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imetoa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi na kuwataka wananchi wa Mwanga kutoa ushirikiano ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

"Shilingi bilion moja za awamu ya kwanza kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya zimeshaletwa na tayari eneo lilikwisha tengwa kwa muda mrefu na linahati miliki na mali ya halmashauri hivyo na mwahidi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwamba tutasimamia vema ujenzi huo ,"amesema Mwaipaya.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe Abdalah Mwaipaya na Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Tadayo wakiongoza baadhi ya wananchi wa Jimbo hilo waliojitokeza kuzindua ujenzi wa hospital ya wilaya hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo akiteta jambo na Mchungaji Abraham Mshana wa  KKKT Dayosisi ya Mwanga Usharika wa Kwamsembea Usangi.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdalah Mwaipaya akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo
Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo akizungumza na vyombo vya habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...