Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imewawezesha wakulima wadogo kupata mikopo ya shilingi bilioni 140 kwa ajili ya kuwainua katika shughuli zao.
Afisa Mwandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Andrew Kimbelwa ametoa taarifa hiyo wakati wa maonesho yanayoenda sambamba na maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani inayofanyika katika viwanja vya nanenane Mkoani Tabora.
Kimbelwa amesema, benki hiyo imekuwa mshirika mkubwa wa ushirika hapa nchini na wametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuendeleza ushirika katika maeneo mbalimbali nchini.
"TADB imekua mshirika wa karibu wa shughuli za ushirika na mpaka sasa tumeishatoa zaidi ya shilingi bilioni 140 kwa ajili ya kuendeleza ushirka"Amesema Kimbelwa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inashiriki maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani ambapo kitaifa yanafanyika Mkoani Tabora
Afisa Mwandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Andrew Kimbelwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...