Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

DIWANI viti maalum,Jimbo la Kibaha Mjini ,ambae pia ni msanii Lydia Mgaya ametoa wimbo Mpya unaoitwa TUMPONGEZE MAMA SAMIA ikiwa umebeba maudhui ya utekelezaji wa masuala mbalimbali nchini yaliyofanyika tangu Rais aanze kuliongoza Taifa.

Anaeleza kwamba,kibao hicho tayari kishatupia kwenye YouTube yake ya Lydia Mgaya.

Diwani huyo msanii wa filamu na mhasibu wa Umoja wa wanawake wasanii Tanzania,mjumbe wa Chama Cha Waigizaji Taifa mstaafu na kamati ya maadili Mkoa wa Kinondoni, alisema licha ya Kuwa kiongozi Lakini hakuna kinachomkwaza kushindwa kuendelea na kazi zake za Usanii.

"Nimeguswa na mama anavyoupiga mwingi ,tumeona namna gani anavyoupambania uchumi wa nchi, kutangaza utalii na uwekezaji nchini, kuwa msikivu kwa wananchi kwa kutatua kero ya maji ,umeme, miundombinu ya barabara na sekta ya elimu ,kupandisha mishahara na posho za watumishi wa Umma ,kumaliza miradi mikubwa ya kimkakati na mengine mengi"anaeleza Lydia .
Alieleza ,yeye Ni msanii wa filamu Lakini ameshaimba nyimbo takriban tatu Sasa upande wa siasa ambapo ameshatoa kibao Cha AMANI ambacho kilielezea namna nchi yetu ilivyo na utulivu na kuwaasa wananchi waidumishe na kumuomba mungu asituingize Kama nchi ya Congo , Ukraine,Urusi na nyingine.

"Baadae hayat Magufuli alipokuwa madarakani pia nilitoa kibao Cha kusifu utekelezaji wa ilani kipindi hicho ,Na sasa nimekuja kivingine ,na wimbo wa Kumsifu SSH na naamini Ni wimbo mzuri na mashabiki wangu wataupenda."

Lydia Mgaya alianza usanii akiwa msichana mdogo alianza kuimba kanisani na kuigiza toka akiwa chipukizi CCM .


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...