Na Karama Kenyunko Michuzi TV

DALARI wa mahakama, Charles Sengo na mfanyabiashara Shabani Kobla wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka 31 yakiwemo ya kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Kija Elias mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Suzan Kihawa imedai, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 26 ya kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma, mashtaka matatu ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hati ya mashtaka Kija amedai, Machi 23 mwaka 2012 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mshtakiwa Kobla kwa makusudi alitoa taarifa za uongo katika kesi ya madai namba 99 ya mwaka 2012 akionesha kwamba Escan Berewell Co Ltd ni kampuni iliyosajiliwa Tanzania wakati akikijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, imedaiwa, Aprili 11 2019, katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam mshtakiwa Kobla akiwa mshindi, mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya Fahak Investment Ltd, kwa udanganyifu alijipatia Sh Milioni 185

Inadaiwa mshtakiwa alijipatia fedha hizo zilizokuwa katika akaunti ya Mahakama Benki Kuu ya Tanzania na kuhamishiwa katika akaunti ya Fahak Investment Ltd fedha ambazo zilitokana na mnada wa hadhara uliofanyika Septemba 11 mwaka 2016 kama ilivyoamriwa katika shauri la mwenendo wa utekelezaji wa hukumu.

Mshitakiwa Kobla pia anadaiwa kujipatia .magari matatu aina Ashock Lyland kwa njia ya udanganyifu kwa madai kwamba yaliuzwa katika mnada wa hadhara.

Kwa upande wa mshtakiwa Sengo yeye anadaiwa kuwa, Juni 20 mwaka 2016, alitoa taarifa za uongo katika Mahakamanya Kisutu kwamba alimuuzia Mariamu Hamadi magari matatu aina ya Layland Ashock kwa nyakati tofauti ambayo yote yana jumla ya thamani ya sh milioni 200.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo pamoja na mambo mengine pia walitakiwa kuwasilisha mahakamani nusu ya kiasi cha cha pesa wanachodaiwa kujipatia.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na wameomba tarehe ya kuwasomea washitakiwa hoja za awali ambapo imepangwa Julai 6 mwaka huu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...