Na Mwandishi Wetu,Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP Jacqueline Kawishe.

Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 30 mwaka huu , 2022 baada ya kufika kwenye ofisini za Spika wa Bunge Mjini Dodoma kwa lengo la kwenda kujitambulisha na kupata ushauri wa Spika hasa kwa kutambua mchango wa Bunge katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya sekta ya uwekezaji.

Akiwa na Spika huyo wa Bunge pamoja na mambo mengine Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP inajihusisha na utengenezaji na utengenezaji na uuzaji wa kiatu cha mtoto wa Shule chenye chapa ya kitanzania ya BARRON, Kawishe ameelezea sababu za kuamua kutengeneza kiatu cha mtoto wa shule ambacho ni bora na kwa gharama nafuu.

“Mheshimiwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tumefika ofisini kwako kwanza kujitambulisha kuwa sisi BARRON GROUP ni kampuni ya Kitanzani iliyoamua kujikita katika kutengeneza kiatu cha mtoto wa shule.

“Tulifanya utafiti na kubaini kiatu cha shule kimekuwa changamoto kwa wazazi na walezi wengi, viatu vya shule vimekuwa na gharama lakini kwa sehemu kubwa vimekosa ubora, sisi tumeamua kuja na kiatu bora na kwa gharama nafuu,”amesema Kawishe.

Mkurugenzi huyo BARRON GROUP akiwa kwa Spika wa Bunge alikuwa ameambatana na Balozi wa kiatu hicho Nasikiwa Byera ambapo pamoja na kujitambulisha wamekabishi viatu vya shule jozi 50 kwa ajili ya Taasisi ya Tulia Trust Foundation.

Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson ( kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP Jacqueline Kawishe( kulia) .Katikatika ni balozi wa kiatu cha shule kinachotengenezwa na kampuni hiyo Nakisiwa Breya

Mkurugenzi wa Kampuni ya BARRON GROUP Jacqueline Kawishe (kulia) akiwa  na Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson baada ya kufika kwa lengo la kujitambulisha kwake pamoja na kukabidhi jozi 50 za viatu kwa Taasisi ya Tulia Trust Foundation. Kushoto ni Balozi wa kiatu cha mtoto wa shule kinachotengenezwa na kampuni hiyo Nakisiwa Breya .Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...