Na Janeth Raphael - Bahi Dodoma

SERIKALI Imekamilisha Ujenzi wa Mradi wa Majisafi katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma utakaohudumia wananchi zaidi ya 17,000 kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 500 fedha zinazotokana na mpango wa ustawi kwa Taifa na mapambano ya athari za UVIKO-19 Eneo la mradi wa maji Wilaya ya Bahi - Dodoma kupatiwa hati miliki

Hayo  yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Antony Sanga akiwa ameambatana na kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti walipotembelea na kujionea mradi wa maji Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, mradi unaotekelezwa na Fedha za UVIKO19 

Mhandisi Sanga amesema mradi huo upo hatua za utekelezaji na kuanzia siku za karibuni Wananchi wa maeneo hayo wataanza Kupata maji.

"Niwaombe wakazi wa Bahi muendelee kujiunganisha, Serikali ya awamu ya sita ipo na nyie na muda si mrefu mnakwenda Kupata maji safi na salama na sisi Wizara tutaisaidia Duwasa kuongeza fedha zaidi ili waendelee na mradi huu na hatutaishia hapa tulipo, nimshuku Rais Samia Kwa kuchukua maamuzi haya ya kuchukua fedha za UVIKO19 zijenge miradi ya maji" - Mhandisi Sanga 

Naye Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti Daniel Sillo amesema anamshukuru Rais Samia Kwa kuona changamoto ya maji katika wilaya ya Bahi na pia amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo Kwa kuhakikisha Wilaya hiyo ya Bahi wanapata maji safi na salama

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA)  Mhandisi Aron Joseph amesema Serikali Kwa kutambua athari za ugonjwa wa UVIKO19 ilitenga fedha za utekelezaji wa mradi wa ujenzi  wa mfumo wa maji eneo la Bahi.

"Duwasa ilipokea fedha kiasi cha milioni 451 Kwa ajili ya kutekeleza mradi huu na kufikisha maji kwa wananchi, DUWASA kupitia makusanyo yake ya ndani pamoja na vyanzo vingine iliongeza milioni 67.4 kugharamia baadhi ya kazi ili kukamilisha mradi huu"- Mhandisi Joseph.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa DUWASA amesema mradi huo unategemea kunufaisha wakazi wapatao elfu kumi na saba (17,000) katika maeneo hayo ya Bahi mjini.

Aidha Mhandisi Joseph ameeleza kuwa mradi huo utaboresha upatikanaji wa maji Bahi Kwa kuongeza lita 528,000 Kwa siku sawa na asilimia 51.7 kwenye Lita 377,000 kwa siku  zinazozalishwa Sasa.

Hata hiyo Mhandisi Aron Joseph ameishukuru Serikali ya awamu ya sita Kwa kuendelea kuisaidia DUWASA katika upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali na uondoshaji maji taka katika jiji la Dodoma pamoja na kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti Daniel Sillo akifungua maji kuashiria kuwa maji yamefika Wilaya ya Bahi Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Antony Sanga, mwenyekiti Daniel Sillo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti Daniel Sillo akipanda juu ya kisima kukagua mradi huo
Katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Antony Sanga Akisalimiana na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti Daniel Sillo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...