Na. Damian Kunambi, Njombe

Wananchi wilayani Ludewa mkoani Njombe wametakiwa kutumia misitu kwa ufugaji wa nyuki badala ya kutumia katika uchomaji mkaa na matumizi mengine ili kuweza kutunza mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.

Wito huo umetolewa na Waziri wa maliasili na utalii Balozi Dkt. Pindi Chana alipokuwa akikabidhi mizinga zaidi ya 300 kwa taasisi na vikundi mbalimbali vya ujasiliamali wilayani Ludewa mara baada ya kufanyika mafunzo ya uhifadhi misitu na vipimo.

Balozi Dk. Pindi Chana asema kuwa shughuli za ufugaji nyuki zinategemea hasa misitu hivyo endapo ufugaji huo utatendeka vyema itasaidia kutunza uhifadhi wa misitu na vyanzo vya maji sambamba na kuinua uchumi wa taasisi na wananchi kwa ujumla kupitia ufugaji wa nyuki.

"Kumekuwa na uharibifu wa misitu kwa kuchoma mkaa, na matumizi mengine. Hii mizinga ina faida kubwa sana katika utunzaji misitu pamoja na kukuza uchumi kwakuwa ili uweze kufuga nyuki unatakiwa uwe na msitu wa kufugia hivyo hii itasaidia uhifadhi wa misitu yetu na kupata kipato kupitia asali" Amesema Balozi Dkt. Pindi Chana.

Aidha kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ameishukuru wizara hiyo na kuvitaka vikundi hivyo kuitumia mizinga hiyo katika kukuza uchumi wao kwakuwa kwa sasa zao la nyuki lipo katika hali nzuri kibiashara.

Ameongeza kuwa ujio wa mizinga hiyo itakuwa msaada kwa taasisi na wajasiliamali kuwa na kazi mbadala ya misitu ambapo badala ya kukata miti ili waweze kupata kipato wataitunza ili waweze kufugia nyuki na kupata faida mara dufu.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa mizinga hiyo Mkuu wa gereza la wilaya ya Ludewa Johanes Baitange ambaye ofisi yake imekabidhiwa mizinga kumi amesema mizinga hiyo itasaidia kutoa elimu ya ufugaji nyuki kwa wafungwa na pindi watakaporejea uraiani wataweza kujipatia kipato kutokana na elimu hiyo walitoipata wakiwa gerezani.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...