Na Evelyne Mpasha, MBARALI

Wakulima wa zao la mpunga wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wametakiwa kuongeza matumizi

ya mbegu bora zilizotafitiwa na Watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ili

kuongeza tija katika uzalishaji wa mpunga na kuachana na kilimo cha mazoea ambacho tija yake

ni ndogo.

Wito huo umetolewa leo (2.07.2022) na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya

ya Mbarali Bwana Geoffrey Mwaijobele wakati akifungua maonesho ya Kilimo Biashara cha

Mpunga yaliyoandaliwa na Kituo cha TARI Uyole kwa kushirikiana na Vituo vya TARI Dakawa na

TARI Ifakara pamoja na Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Mpunga (IRRI). Maonesho hayo

yamefanyika katika Kata ya Ubaruku Wilayani Mbarali iliyoko mkoa wa Mbeya.

Katika hotuba yake, Mwaijobele ameipongeza TARI kwa kuleta matokeo ya utafiti wa zao la

Mpunga karibu na wananchi hususan katika Wilaya ya Mbarali na kutoa elimu kwa wakulima.

Elimu iliyotolewa katika maonesho ya kilimo biashara cha mpunga ni pamoja na sifa za mbegu

mpya za mpunga, maandalizi ya shamba, matumizi bora ya mbolea, palizi na hatua za uvunaji

hatua ambayo itasaidia wakulima wa Wilaya ya Mbarali na maeneo mengine yanayofaa kwa

kilimo cha mpunga kulima kisasa, kuwa na uhakika wa chakula na ziada ya kuuza kwa ajili ya

maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla .

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Uyole ambaye Dkt. Denis Tippe alieleza kuwa

Kituo cha TARI Uyole kiliweka majaribio ya mbegu mpya sita katika skimu ya umwagiliaji Kata ya

Ubaruku Wilayani Mbarali ili kuongeza matumizi ya mbegu bora za mpunga na kuliongezea tija

baada ya kubaini changamoto iliyopo ya kushuka kwa tija katika uzalishaji wa zao hilo.

Dkt. Tippe aliongeza kuwa mbegu hizo mpya za mpunga za SARO 5, TARI RIC 1 & 2, Komboka,

SATO 1 & 9 ambazo zina sifa za kutoa mavuno mengi kuanzia tani 7.5 hadi 8.5 kwa hekta,

kunukia, kuwa na punje nzuri, kukomaa kwa muda mfupi na baadhi zinavumilia maeneo

yaliyoathiriwa na magadi na chumvi chumvi zimeonyesha kufanya vizuri katika majaribio

yaliyoandaliwa kwa ajili ya maonesho hayo ambayo yanalenga mkusaidia mkulima kuchagua

mbegu ambayo itamfaa kulingana na eneo lake.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TARI aliyehudhuria maonesho hayo

Dkt. Richard Kasuga amesema maonesho hayo ni moja moja ya majukumu muhimu ya TARI ya

kuhakikisha teknolojia zinazotafitiwa zinawafikia wakulima na wadau wa kilimo kupitia njia

mbalimbali za mawasiliano ikiwemo maonesho ya kilimo biashara, vituo mahiri, vyombo vya

habari na mitandao ya kijamii. Aliongoeza kuwa matumizi ya mbegu bora za mpunga zitasaidia

kuongeza uzalishaji na hivyo kufikia malengo ya Serikali ya kujitosheleza kwa chakula na pia

Malengo ya yaliyoainishwa katika Azimio la Malabo la kukabilana na njaa.

Akizungumzia kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Kasuga ameongeza

kuwa katika mwaka wa 2022/2023 bajeti ya maendeleo ya utafiti imeongezeka kutoka takriban

bilioni 11 hadi billion 41.


Ameongeza kuwa, Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe ameweka mkazo na malengo

ya AJENDA 10/30 yenye kaulimbiu KILIMO NI BIASHARA yenye lengo la kujitosheleza kwa

chakula na ziada kwa ajili ya kuuza na kujiongezea kipato, Hivyo maonesho haya ni fursa katika

kuwahamasisha wakulima kutumia fursa za masoko ambalo Wizara imeendelea kuyatafuta

ikiwemo la Ubeljiji kwa ajili ya kuuza mchele.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wakulima wa zao la mpunga Wilayani Mbarali wameipongeza

na kuishukuru TARI kwa kuwezesha kuweka majaribio ya mbegu mpya za mpunga Wilayani

humo na kuuomba Uongozi wa Wilaya ya Mbarali kuwaletea wataalamu wa TARI karibu yao ili

waweze kuwasaidia kuwapimia afya ya udongo na kuwapa elimu zadi ya matumizi ya mbegu

mpya, matumizi sahihi ya udongo pamoja na ushauri ili waweze kupata tija zaidi katika kilimo

chao ikiwa ni pamoja na kuwa na uhakika wa uwepo wa mbegu hizo Wilayani Mbarali.

Wakulima hao wameeleza kuwa muda wote walikuwa wakilima kilimo cha mazoea ambacho

hakikuwa na tija kwani walikuwa wakipata gunia 8 -10 kwa ekari moja, lakini sasa wanataka

kubadilika na kutumia mbegu mpya za TARI ambazo humuwezesha mkulima kupata kati ya

gunia 30 - 40 kwa ekari moja.

Wakulima waliohudhuria maonesho hayo ya Mpunga Kilimo Biashara wametoka katika vijiji vya

Ubaruku, Kapunga, Madibila, Uturo na Buyuni Wilayani Mbarali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...