Wawekezaji kutoka Nchi za falme za kiarabu wakitazama matunda ya Parachichi mara baada ya kuvunwa katika shamba la mkulima mjini Njombe.
Wawakezaji wakiwa katika shamba la matunda ya Parachichi la bwana Nemes wa halmashauri ya mji wa Njombe walipofika mkoani Njombe kwa jailli ya kujifunza kilimo cha matunda ya Parachichi.
Muwekezaji akiwa kwenye picha ya pamoja na bwana Nemes Mkulima wa Parachichi mjini Njombe katika miche yake ya Parachichi walipotembelea mkoani Njombe.

Njombe
SERIKALI nchini Tanzania imepokea wawekezaji kutoka nchi za falme za kiarabu wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo kilimo cha Parachichi katika mkoa wa Njombe.

Mbunge wa Afrika Mashariki Bi,Fancy Nkuhi akiiwakilisha nchi ya Tanzania amesema wawekezaji hao wamewasili nchini na kufika katika mkoa wa Njombe kwa nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha Parachichi huku akibainisha kuwa ugeni huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia aliyoifanya nchini Oman wiki mbili zilizopita.

“Nimekuja na wageni ambao wanatoka nchi za falme za kiarabu ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sao la Parachichi kwenye mkoa wa Njombe,huu ni muendelezo wa kazi kubwa aliyoifanya Mh,Rais kwenye Ziara yake na filamu ya Royal tour”alisema Nkuhi

Kwa mujibu wa kampuni ya BACOIN ya nchini Tanzania iliyofanikiwa kufika na wawekezaji hao mkoani Njombe imebainisha kuwa nia ya wawekezaji hao sambamba na kilimo cha Parachichi ni kufanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa kiwanda cha Nyama huku katika sekta ya utalii wakiwa na malengo ya ufugaji wa farasi.

Judica Omary ni katibu tawala wa mkoa wa Njombe kwa niaba ya mkuu wa mkoa Waziri Kindamba amesema serikali ya mkoa huo ipo tayari kuwapokea wawekezaji hao huku akihakikisha ushirikiano pamoja na upatikanaji wa ardhi.

“Nia ya uwekezaji wa hawa wageni wanahitaji ekari 100,0000 inabidi kwa mkoa wetu wa Njombe tuwapeleke katika maeneo mbali mbali,kitu kikubwa kilichonifariji ni kwa kuwa wana nia ya kuwekeza katika mazao mbali mbali”amesema Judica Omary

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...