Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL,) Mhandisi. Ladislaus Matindi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kampuni  ya  uwakala wa tiketi za ndege ya  Skylink Travel and Tours, kulia ni    Mkurugenzi wa kampuni ya Skylink travel,Moustafa khataw

 

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL,) limesema litaendelea kuboresha huduma mbambali za shirika hilo ikiwemo kuongeza safari nyingi za nje ya nchi ili kuweza kuendana na soko la kimataifa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi mara baada ya kutembelea  kampuni  ya  uwakala wa tiketi za ndege ya  Skylink Travel and Tours iliyopo jijini hapo.

Matindi amesema baada ya kufanya vizuri kwenye soko la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sasa wanajiandaa kwenda nchi za Afrika magharibi hapo mwakani baada ya ujio wa ndege tano hivyo jambo lilopo sasa kwa ATCL ni kutatua changamoto  zinazoikabili.

Aidha,Matindi amesema kwa sasa wamebaini kuna changamoto kwenye suala la tiketi ikiwemo abiria kuchelewa kupata tiketi zinazochangiwa na kusuasua kwa baadhi ya kampuni za ukataji tiketi na kuzitaka  kampuni hizo kutatua changamoto hiyo kwa kuwataka wateja kuweka umakini katika ukataji tiketi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Skylink Travel, Moustafa Khataw amesema wamemweleza Mhandisi. Matindi kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuzidisha vituo vya Air Tanzania katika vituo vya kimataifa na wameafikiana kwamba watakua wanakutana ili kuzungumza na kubadilishana mawazo kwaajili ya Air Tanzania kwa ujumla.

Pia Khataw alihakikisha kuwa mawakala wa Air Tanzania watashirikiana na Air Tanzania ili kupata muafaka mzuri wa kupanua biashara kwa ujumla.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...