Na Mwandishi Wetu, Michuzi Blog - Rombo

 
KATIBU MKuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Daniel Chongolo ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya Shule mpya iliyopo Kata ya Mamsera katika Tarafa ya Mengwe wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro

Akiwa katika shule hiyo leo Agosti 5,2022 , Chongolo ameeleza kufurahishwa na ujenzi wa shule hiyo na kutoa pongezi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali hasa waliokuwa wakisimamia ujenzi huo kwani umefanyika kwa kiwango cha kuridhisha.

Akizungumza mbele ya wana CCM na wananchi wa maeneo hayo Chongolo amewahakikishia kwamba yote yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Chama hicho na ambayo yapo katika meza yake Mwenyekiti wao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya utekelezaji yatatekelezwa kama yalivyoahidi

" Ilani imeahidi elimu na ninyi ni mashahidi Rais na Serikali anayoiongoza imeshapeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule. Ilani imeahidi na Serikali inafanya kazi kubwa katika maeneo hayo na maeneo mengine.

"Ndugu zangu viongozi na ndugu wananchi Chama Cha Mapinduzi kiliomba ridhaa ya kuongoza nchi hii na kikapewa dhamana ya kuongoza katika kipindi cha miaka mitano, sasa tuko mwaka 2022 tuna mengi ambayo tuliahidi na tunaendelea kuyafanyia kazi moja baada ya jingine.

"Tuliahidi na wanaotenda ni Serikali, sisi kama Chama ambacho tunadamira ya kuongoza nchi kwa kipindi kerefu hatuwezi kukaa pembeni tukaacha mambo yaende kienyeji ndio maana tunapita kila eneo kwenda kuona kama mambo yanakwenda sawa sawa ,nipongeze kamati iliyosimamia na kuratibu ujenzi wa shule hii ,tumepita tumeangalia miundombinu na tumeridhika,"amesema Chongolo.

Aidha amesema pamoja na umuhimu wa madarasa ni muhimu kuwa na viwanja vya michezo kwasababu ni sehemu ya elimu, hivyo wanataka mtoto acheze na asome kwa mujiibu wa ratiba zilizopo na mimi kuweka mtihani huo naacha mipira niliyopewa na Mwenyekiti wao.

"Tafuteni uwanja wa michezo kwani michezo inasaidia mambo mengi,baada ya muda wa masomo watoto watakuwa wanakwenda kucheza.Nipongeze pia menejimenti ya Halmashauri lakini niipongeze kamati ya ulinzi na Usalama kwani wakati tunakagua miundombinu kila mtu alikuwa anajua kinachoendelea hicho ndicho tunachotaka.

"Lakini nimefurahishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ambaye amejiridhisha na ujenzi huu na fedha ya Serikali kufanya kazi kama inavyotakiwa.Hatuwezi kuwa kwenye maeneo fedha nyingi zinashushwa halafu tunakaa nazo kienyeji, tunaacha hazileti matokeo yaliyokusudiwa kwa Wananchi."

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza mbele ya Wananchi na Wanachama wa CCM (hawapo pichani) baada ya kukagua  mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdini Babu akizungumza mbele ya Wananchi na Wanachama wa CCM (hawapo pichani) baada ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kukagua  mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maeleo mafupi wakati alipotembelea mradi ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Mamsera Kati ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...