Na Khadija Kalili, CHALINZE
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah amewaambia Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze kuwahi fursa za kuwekeza katika eneo la Bandari Kavu ya Kwala.

"Huu ni wakati wenu wa kukaa na kujiwekea mikakati ya kulitazama eneo la uwekezaji la Bandari Kavu ya Kwala mapema na kulipanga vinginevyo mkichelewa litavamiwa kwa sababu wanakijiji watauza kiholela jambo ambalo halitakuwa na faida tofauti na Halmashauri husika endapo itasimamia zoezi la upangaji wa maeneo kwa kuzingatia huduma husika hivyo changamkieni hii fursa."

Watu wanakimbilia katika eneo la Kwala kwa sababu ya kujenga viwanda hii ni fursa kubwa ya kiuchumi ndani ya Halmashauri ya Chalinze hivyo tuwekeze kwa moyo mmoja na kujipanga ipasavyo yaani Chalinze umasikini utakuwa basi.

Tuwekeze kwa kujenga maduka makubwa na makazi ya watu Chalinze itabadilika.

DC Zainab aliwaambia Madiwani hao leo Agosti 12 alipozungumza katika kikao cha Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na shughuli zinazofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya mwaka wa fedha 2021/22.

Alisema kuwa wasione shida kutoa kiasi kikubwa cha fedha hata kama ni Mil.20 ambapo zitatumika katika kuwekeza kwa kupanga Viwanda vitakuwa wapi kwa sababu watakuwa wamewekeza katika eneo hilo na fedha hiyo itarudi.

Amesema kuwa lazima tupange malori yatakaa wapi, viwanda vitakaa wapi kwa sababu malori yatakuwa mengi yakipakua na kupakia mizigo kutoka katika Bandari kavu ya Kwala eneo ambalo litakuwa eneo kubwa la kibiashara na fursa kubwa kiuchumi.

"Sisi Halmashauri ya Chalinze kama tutawekeza mapema katika huu Mradi wa Kwala umasikini kwetu utaondoka na kubaki historia kwa viongozi na wananchi wake kwa ujumla." Amesema Zainabu

Natoa rai kwa umeme Shirika la Umeme TANESCO tusogeze nguzo za umeme katika lile eneo Kwala, DAWASA pelekeni maji, TARURA kachongeni barabara hata kama hazitakuwa za kiwango cha lami ili wawekezaji wakija kuangalia eneo liwavutie kutokana na kuona kuna miundombinu rafiki ya uwekezaji.

"Mimi nina uhakika kuwa kwa mpango wa serikali ambapo wamepanga mradi huu uanze ifikapo Desemba mwaka huu wanataka kuona utekelezaji wa Mradi huu wa Kwala uwe umeanza na kama alivyosema Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge kuwa kuna wawekezaji ambao wanakuja kujenga viwanda 100 hawa wote kila siku wanakula wanavaa sasa hizi huduma zote zitakuza uchumi." 
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah akizungumza 
katika kikao cha Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na shughuli zinazofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya mwaka wa fedha 2021/22.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Hassan Mwinyikondo akizungumza katika kikao cha Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na shughuli zinazofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya mwaka wa fedha 2021/22.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...