Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la EWURA katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

*Serikali yatoa ruzuku tena ya bilioni 100 kupunguza makali kwa wananchi kupata nishati hiyo.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za
bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini ambapo bei hizo zimeanza kutumika kuanzia Agosti 3, 2022 lengo ni kutaka wananchi wapate huduma bora bila ya kuwepo ongezeko la holela.

Akizungumza na Michuzi Blog kwenye maonesho ya Kilimo Kitaifa Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Titus Kaguo amesema kuwa bei za Mafuta katika soko la dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia na ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya bilioni 100 kwa ajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa Agosti 2022.

Amesema kuwa Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Agosti 2022 ambapo bei hizo zinatofautiana kutokana na umbali kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kadri ya umbali unapokuwa mrefu ruzuku yake inakuwa kubwa.

Kaguo amesema kuwa Bei za Mafuta kwa mwezi Agosti 2022 kabla na baada ya ruzuku
Agosti 2022 Bei kabla ya ruzuku, Agosti 2022 Bei baada ya ruzuku pamoja na Kiwango cha Ruzuku kwa Petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam bei petroli 3636 baada ya ruzuku 3410 kiwango cha ruzuku 220 hivyo mfano huo kwa Mkoa huo inaonyesha sehemu nyingine beo zinapanda kutokana na umbali.

Amesema kuwa katika kutekeleza bei hizi, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta watatakiwa kuzingatia kwa EWURA kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za

Mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

Amesema kuwa Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko na EWURA hiyo itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Amesema taarifa zinazotolewa lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta na Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za kupanga bei za Mafuta za mwaka 2022 zilizotangazwa.

Amesema vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika pale ambapo

inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja.

Aidha amesema adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika na Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye Mashine za EFPP na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. 

Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.

Hata hivyo amesema kuwa Wauzaji wa Mafuta ya petroli wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiu agizo hilo.

Amesema Wauzaji wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...