Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,akizungumza wakati wa  warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI  89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,akisisitiza jambo kwa washir8iki wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI  89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,(hayupo pichani) wakati wa  warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI  89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.9 ikiwa ni ruzuku kwa baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

BAADHI ya waliokabidhiwa  mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.9 ikiwa ni ruzuku kwa baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa ruzuku hiyo  leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo,akielezea jinsi fedha zitakazofanya kazi katika jamii mara baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kukabidhiwa bilioni 4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa ruzuku hiyo  leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TAWSEI kutoka Mkoa wa Tanga, Bernadethe Choma,akizungumza mara baada ya kuwa mmoja wapo wa asasi za kiraia zitakazo pokea ruzuku za FCS kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa ruzuku hiyo  leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

.........................................

Na Alex Sonna-DODOMA

SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS), limetoa ruzuku ya Sh.Bilioni nne kwa Asasi za Kiraia (AZAKI) 89 kwa Tanzania bara na visiwani ili kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya program ya utawala bora katika sekta za maji,elimu afya na kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga,wakati wa  warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba.

Amesemwa kuwa  FCS imejikita katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha maisha yao na kukuza  sekta ya asasi za kiraia.

“Tumepata wadau 89 wanaotoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar na kazi kubwa itakayofanyika ni kusukuma ajenda ya utawala bora hapa nchini,”amesema.

Bw.Kiwanga amesema kuwa eneo  jingine la utawala bora ni vita dhidi ya kuondoa ukatili wa kijinsia lakini pia kundi la vijana, kuhakikisha rasilimali zinazotolewa na serikali na wadau wengine, kweli ziwafikie makundi hayo na watu wenye mahitaji maalum.

Pia katika sekta za  elimu, afya na kilimo, usawa wa kijinsia, ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.

“FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao.

Kiwanga amesema  kuwa kumekuwepo ongezeko la migogoro katika rasilimali hivyo kwa sasa kuna taasisi 10 zitafanya kazi ya kuitatua hususani maeneo ya Kusini, Morogoro na Kilosa.

Amesema FCS imeweka mfumo madhubuti wa kuhakikisha  kila shilingi inatumika kwa lengo lilokusudiwa huku  taasisi zizofuata utaratibu watachukua hatua kali.       

Kwa upande wake ,Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo amesema  FCS wanafanya kazi na mashirikia madogo  ambao ni wabia na viongozi wa klasta za programu wambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa.

Amesema wanafanya kazi na asasi za kijiji, kata na wilayani huku wabia ni mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu.

Chilimo amesema  mashirika yanayofadhiliwa na FCS sio waruzukiwa tu, ni wabia pia na kwamba baadhi ya misingi ya ubia ni uelewa wa pamoja,malengo ya pamoja, na kuaminiana ili kuweza kufikia malengo ya pamoja.

“Tumekuwa walezi wa sekta ya AZAKI, tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TAWSEI kutoka Mkoa wa Tanga, Bernadethe Choma,amesema wao kama NGO’S kupitia ruzuku wanazopewa zitaenda kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo husika.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...