Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Hassan Mwinyikondo akizungumza wakati wakati alipokuwa akizungumza katika Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na miradi na shughuli zilizofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2021/22.

Na Khadija Kalili, CHALINZE
HALMASHAURI ya Chalinze Mkoani Pwani imejipanga kutoa elimu ya kuhamasisha wakazi wake kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kufanya matembezi ya hisani yakiambatana na Tamasha la Michezo mbalimbali ikiwemo jogging na Mpira wa miguu ambapo watashirikiana na Wilaya ya Kipolisi Chalinze.

Mbali ya jogging pia watacheza mechi ya mpira wa miguu itakayo wakutanisha timu ya Halmashauri ya Chalinze timu ya Wilaya ya Kipolisi Chalinze.

Tamasha hilo litafanyika Agosti 23 mwaka huu.

Mwenyekiti huyo alisema hayo leo Agosti 11 wakati alipokuwa akizungumza katika Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na miradi na shughuli zilizofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2021/22.

Mwinyikondo alisema kuwa hivi sasa Chalinze wanatembea na Kauli mbiu isemayo 'Mimi Niko Tayari kihesabiwa je wewe'.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhan Possi amewashukuru Madiwani wote kutokana na ushirikiano wao katika mwaka wa fedha uliopita ambapo wamechangia kuleta matokeo mazuri kwa kuwa chachu ya maendeleo kwa kushika nafasi ya pili nchi nzima katika ukusanyaji wa mapato kati ya Hamashauri 185 nchi nzima kwa kukusanya mapato kwa asilimia 60 huku Jiji la Dodoma ikiongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 61.

Alisema kuwa madiwani wasimamie bajeti tuweze kuisaida serikali katika kukuza uchumi huku akisema kuwa Halmashauri ya Chalinze katika mwaka wa fedha ujao imejipanga kukusanya kiasi Cha Bilioni 13.6 ambapo pia wataimarisha ukusanyaji kodi katika kutoa huduma.
Mkurugenzi Halmashauri ya Chalinze Ramadhan Possi akizungumza wakati alipokuwa akizungumza katika Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na miradi na shughuli zilizofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2021/22.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhan Possi akisikiliza mada wakati alipokuwa akizungumza katika Baraza la Kata la kuwasilisha taarifa za Kata zinazohusiana na miradi na shughuli zilizofanywa na Halmashauri ya Chalinze ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2021/22.
Baadhi ya Madiwani wakiwa katika kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...