Mwandishi wetu, Arusha


Mchezaji wa Golf Jay Nathwani wa klabu ya Gymkhana Arusha, ameshinda mashindano ya Golf ya Arusha open 2022 yaliyofanyika uwanja wa Gymkhana jijini Arusha.

Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bima ya Reliance na kishirikisha wachezaji 117.

Nathwani ameshinda kwa kupata jumla ya mikwaju 154 na nafasi ya pili ilichukuliwa na aliyekuwa bingwa mtetezi wa mashindano hayo Victor Joseph wa kutoka klabu ya Gmykhana ya jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mashindano hayo,Prudence Kaijage amemtangaza mshindi kwa upande wa wasichana alikuwa ni Neema Ulomi akifuatiwa na Stella Emmanuel.

Kaijage amesema kwa upande wa watoto mshindi alikuwa ni Mohamedasad Meloncelli huku katika daraja la A, mshindi alikuwa ni Aliabbas Kermali akifatiwa na Nathaniel Itinda, huku Raju Ladhia akishinda upande wa daraja B akifatiwa na Dismas Seth na daraja C ameshinda Dian Vaja akifuatiwa na Tinka Sour.

Akizungumza katika hafla ya kutoa zawadi, Mtendaji mkuu kampuni ya ya bima ya Reliance Ravi Shankar ameahidi kampuni hiyo kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka ili kukuza mchezo wa golf nchini.

Shankar amesema kampuni hiyo imefarijika kuona idadi ya washiriki hasa wanawake na vijana inaongezeka kutoka mwaka jana ambapo washiriki walikuwa 104 tu.

Mkuu wa idara ya masoko ya kampuni ya bima ya Reliance, Joyce Bendera amesema mwaka huu idadi ya wanawake imeongezeka na kufikia 13 na watoto 24.

"tunapenda kutoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapa fursa watoto wao kujitokeza kucheza mchezo huu na Golf kwani ni mzuri," amesema.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi aliyekuwa mgeni rasmi, Mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Mrisho Gambo amewapongeza washiriki wote katika mashindano hayo kwani pia yanachangia kukuza utalii katika jiji la Arusha.

"Tunapongeza kampuni ya bima kuendelea kudhamini kwa mwaka wanne sasa mashindano haya ambayo yanakutanisha wachezaji kutoka Afrika ya Mashariki na kwa Arusha ni fursa ya kukuza Utalii na biashara" amesema.

Mwenyekiti wa Gymkhana klabu Julius Karata amepongeza klabu sane ambazo zilishiriki mashindano hayo.

Amezitaja klabu hizo kuwa ni Lugalo na Gymkhana za Dar es Salaam, Gymkhana Arusha, TPC, Moshi Golf, KiliGolf, Uganda Golf na klabu ya Kenya .





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...